Pata taarifa kuu

Kocha wa Barcelona Ronald Koeman kuwaaga wachezaji wake

Kocha wa Klabu ya Barcelona,  Ronald Koeman amefutwa kazi, miezi 14 baada ya kuanza kuifunza klabu hiyo. Katika mechi 10 ambazo ameongoza Barcelona, ameisaidia klabu hiyo kupata alama 15, na tayari imepoteza mechi mbili za hatua ya makundi, hatua ya klabu bingwa barani Ulaya.

Kocha wa Klabu ya Barcelona,  Ronald Koeman.
Kocha wa Klabu ya Barcelona, Ronald Koeman. LLUIS GENE AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumtano, Barcelona ambayo ni ya tisa kwa alama sita, ilifungwa na Rayo Vallecano bao 1-0 na leo anatarajiwa kuwaaga wachezaji wa Barcelona.

Koeman, 58, aliajiriwa na Barcelona kwa mkataba wa miaka miwili mwanzoni mwa msimu wa 2020-21 na ameongoza kikosi chake kusajili matokeo mseto kwenye mapambano mbalimbali ya hadi kufikia sasa msimu huu.

Awali vyombo vingi vya habari nchini Uhispania viliripoti kwamba Koeman ambaye ni raia wa Uholanzi, atatimuliwa na Barcelona iwapo atashindwa kuongoza kikosi hicho kutia kapuni ufalme wa angalau taji moja msimu huu.

Kocha huyo anaondolewa baada ya kutumikia Barcelona kwa miezi 14, lakini ameandamwa na matokeo mabaya msimu huu ambapo amekusanya alama 15 pekee katika mechi 10 za Ligi Kuu ya Hispania na michezo minne ya mwisho amepoteza mitatu huku akichagizwa na kipigo katika El Classico dhidi ya Real Madrid.

Koeman amekutana na changamoto kubwa ambapo klabu inapitia kipindi kigumu cha kiuchumi,na kikubwa alichokifanya ni kuifanya Barcelona kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu msimu uliopita na pia kutwaa kombe la Mfalme.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.