UINGEREZA
Klabu zitakazomenyana hatua ya nusu fainali kuwania taji la Carabao zafahamika
Nchini Uingereza, Arsenal itamenyana na Liverpol katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la Carabao.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Katika nusu fainali nyingine, Chelsea itamenyana na Tottenham Hotspurs, mechi ambayo itakuwa kama fainali ya mwaka 2015 wakati timu hizi zilikutana na The Blues wakaibuka mabingwa kwa kuishinda Spurs mabao 2-0.
Mechi hizo za nusu fainali zitachezwa nyumbani na ugenini mwanzoni na katikati ya mwezi Januari huku fainali ikipigwa Februari 27 katika uwanja wa Wembley.
Matokeo ya michuano ya robo fainali
Arsenal 5-1 Sunderland
Brentford 0-2 Chelsea
Liverpool 5-4 Leicester City
Tottenham Hotspurs 2-1 West Ham United