Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO

Senegal kupepetana na Misri katika fainali ya michuano ya Kombe la Afrika

Misri ilikatiza ndoto ya Cameroon ya ushindi nyumbani kwa kushinda nusu-fainali kati ya washindi wawili wakubwa barani Afrika (0-0, 3 kwa 1), Alhamisi mjini Yaoundé, na hatimaye itamenyana na Senegal siku ya Jumapili.

Misri wakifurahia ushindi wao kupitia mikwaji ya penalti dhidi ya Cameroon kwenye uwanja wa Olembé mjini Yaoundé, Februari 3, 2022.
Misri wakifurahia ushindi wao kupitia mikwaji ya penalti dhidi ya Cameroon kwenye uwanja wa Olembé mjini Yaoundé, Februari 3, 2022. © FMM/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya soka ya Misri imewashinda wenyeji Cameroon mabao 3 kwa 1 kupitia mikwaju ya penalti na kufuzu fainali ya kutafuta kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Senegal siku ya Jumapili.

Baada ya mechi hiyo ya nusu fainali kuisha kwa timu zote, kutofungana katika muda wa kawaida na ule wa ziada, mikwaju ya penalti ilipigwa kuamua mshindi.

Kipa wa Misri Mohamed Abou Gabal ndiye aliyekuwa shujaa wakati wa upigaji wa penalti, baada ya kuzuia mikwaju miwili kutoka kwa Cameroon, huku mchezaji mwingine Clinton Njie akipiga  nje.

Senegal inawania taji la kwanza, baada ya fainali mbili kushindwa (2002 na 2019), Misri ikiwa ya nane, ili kuendeleza rekodi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.