Pata taarifa kuu

Msimu mpya katika klabu ya Barcelona Busquets akistaafu

NAIROBI – Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez anaamini msimu mpya na ukurasa mpya unafunguliwa na Klabu hiyo yenye maskani yake jijini Catalunya Hispania.

Sergio Busquets anatarajiwa kuondoka Barcelona
Sergio Busquets anatarajiwa kuondoka Barcelona AP - Joan Monfort
Matangazo ya kibiashara

Maneno ya Xavi yanajiri baada ya nyota mkongwe kiungo kati Sergio Busquets kusema wiki hii ataondoka msimu wa joto mwishoni mwa kandarasi yake.

Kiungo huyo raia wa Hispania alikuwa sehemu muhimu katika kikosi kilicholeta mafanikio mengi uwanjani campnou.

Busquets alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ligi ya mabingwa mara tatu, na anaweza kutwaa taji lake la tisa la La Liga ikiwa Barcelona wataifunga Espanyol Jumapili.

Sergio Busquets wa Barcelona
Sergio Busquets wa Barcelona AP - Alvaro Barrientos

Pia alicheza kama mhimili mkubwa nyuma ya Andres Iniesta na Xavi katika safu ya kiungo ya tatu, na watatu hao pia walishinda Kombe la Dunia wakiwa na Uhispania mnamo 2010.

Hata hivyo kocha Xavi anasema anatumai wachezaji kama Pedri na Gavi wangeweza kushinda chochote yeye, Iniesta na Busquets wangefanikisha Barcelona.

"Tunajitahidi kuunda (msimu) mpya," Xavi aliambia mkutano wa wanahabari Jumamosi.

"Natumai wachezaji kama Gavi, na Pedri, wanaweza kwenda zaidi yetu, hayo ni maisha, huo ni mchezo.

Xavi Hernandez
Xavi Hernandez AP - Jose Breton

Busquets mwenye umri wa miaka 34, ameichezea Barcelona zaidi ya mara 700 na kubeba mataji 31. Hata hivyo nafasi yake ya juu zaidi katika tuzo la Ballon d'Or ilikuwa ya 20, mwaka 2012.

"Yeye ndiye kiungo bora zaidi wa ulinzi ambaye nimewahi kuona," aliendelea Xavi.

"Kutoteuliwa kwa Ballon d'Or, kwangu ilikuwa dhuluma."

Sergio amesifiwa kwa kuleta tajiriba katika kikosi cha Barcelona
Sergio amesifiwa kwa kuleta tajiriba katika kikosi cha Barcelona AFP

Busquets alisema hapo awali anapendelea kuangazia fedha badala ya sifa za kibinafsi na Jumapili inawapa Barcelona nafasi ya kushinda La Liga kwa mara ya kwanza tangu 2019.

"Tuko na asilimia 200 ya kushinda," Xavi alisema kabla ya mpambano na wapinzani wa Catalan derby Espanyol huko Cornella.

Iwapo Barcelona itashinda mechi hio watatawazwa mabingwa wa msimu wa mwaka 2022 -23 wa Laliga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.