Sevilla ndio mabingwa wa ligi ya Europa 2023
NAIROBI – Sevilla wameshinda taji la saba la ligi ya Europa baada ya kuwashinda Roma kwa mikwaju ya penalti kwenye uwanja wa Puskas Arena mjini Budapest.
Imechapishwa:
Gonzalo Montiel, ambaye pia alifunga penalti ya ushindi kwa timu ya taifa ya Argentina katika fainali ya Kombe la dunia dhidi ya Ufaransa nchini Qatar, aliifungia klabu yake ya Uhispania kufuatia sare ya 1-1.
Roma ya Uhispania, sasa imeshinda fainali zote saba walizocheza katika mashindano hayo huku nahodha Jesus Navas akishiriki katika ushindi wao wa kwanza dhidi ya Middlesbrough mnamo 2006.
Hatua hii inawafanya kufuzu kwa ligi ya mabingwa msimu ujao licha ya kumaliza nje ya nne bora kwenye La Liga.
Jose Mourinho kocha wa Roma alikuwa ameshinda fainali zote tano za awali za Europa alizoshiriki. Paulo Dybala aliiweka Roma mbele katika kipindi cha kwanza. Nao Sevilla walisawazisha katika dakika ya 10 baada ya kipindi cha mapumziko.
Roma bila shaka walipata fursa nzuri zaidi za kushinda mechi hiyo katika muda wa kawaida huku Tammy Abraham na Ibanez wakikosa nafasi nyengi.