Pata taarifa kuu

Messi kuondoka PSG wikendi hii

NAIROBI – Klabu ya PSG imethibitisha kuwa nyota wa Argentina Lionel Messi ataondoka katika klabu hiyo ya nchini Ufaransa siku ya Jumamosi.

Inadaiwa kuwa huenda Lionel Messi akahamia Saudi Arabia baada mkataba wake kukamilika PSG
Inadaiwa kuwa huenda Lionel Messi akahamia Saudi Arabia baada mkataba wake kukamilika PSG © AFP - FRANCK FIFE
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, kocha wa PSG Christophe Galtier, alieleza kuwa mechi yao dhidi ya Clermont siku ya Jumamosi ndio itakuwa ya mwisho kwa mchezaji huyo ambaye mkataba wake unakamilika mwishoni mwa Juni.

"Nilikuwa na fursa ya kufundisha mchezaji bora zaidi katika historia ya soka," Galtier alisema. "Hii itakuwa mechi yake ya mwisho katika Parc des Princes, na ninatumai kwamba atapokelewa vyema."

Kocha wa PSG Christophe Galtier
Kocha wa PSG Christophe Galtier AFP - ANNE-CHRISTINE POUJOULAT

PSG ilimsajili Messi mnamo Agosti 2021 wakiwa na nia  kushinda Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ndoto ambayo ingali inasubiriwa kutumia.

Japokuwa PSG ilishinda taji lake la 11 la ligi ya Ufaransa wikendi iliyopita, iliondolewa katika michuano ya kuwania klabu bingwa katika hatua ya 16 bora.

Mshindi huyo mara saba wa Ballon d'Or alionekana kuimarika msimu huu kutokana na mwingiliano mzuri na  Kylian Mbappe uwanjani.

Lionel Messi ameonekana kuwa na mwingiliano mzuri  na Kylian Mbappé msiumu huu
Lionel Messi ameonekana kuwa na mwingiliano mzuri na Kylian Mbappé msiumu huu AP - Christophe Ena

"Mwaka huu, amekuwa mchezaji muhimu kwa  timu, anapatikana kila wakati, anajitolea kila wakati wakati kwenye mazoezi," Galtier alisema. "

Mwezi uliopita, klabu hiyo ilimzuia kucheza mechi kadhaa kufuatia safari isiyoidhinishwa ya kwenda Saudi Arabia. Messi ana mkataba wa kibiashara na Saudi Arabia wa kutangaza utalii na amekuwa akihusishwa na kuhamia huko mwishoni mwa msimu.

Lionel Messi amehusishwa na Saudi Arabia ambako Cristiano Ronaldo anacheza
Lionel Messi amehusishwa na Saudi Arabia ambako Cristiano Ronaldo anacheza © FRANCK FIFE / AFP

Pia kumekuwa na mazungumzo ya kurejea Barcelona, ​​ambapo alitumia muda mwingi katika taaluma yake ya soka, au Marekani kucheza MLS.

Messi aliwasili Barcelona akiwa na umri wa miaka 13 na kuondoka akiwa ameshinda mataji 35. Aliisaidia klabu hiyo kushinda Ligi ya Mabingwa nne, ligi 10 za Uhispania, na Copa del Reys saba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.