Pata taarifa kuu

Thomas Partey: Mikel Arteta anasema kiungo wa Arsenal atasalia Emirates

Nairobi – Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anasema anatarajia kiungo Thomas Partey kusalia katika klabu hiyo ya ligi kuu ya Uingereza, licha ya kutokuwa na uhakika juu ya mustakabali wake.

Kocha wa Arsenal anaamini mchezaji huyo atasalia katika klabu hiyo
Kocha wa Arsenal anaamini mchezaji huyo atasalia katika klabu hiyo AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Nyota huyo wa Ghana alichelewa kujiunga na kikosi cha The Gunners kwa ziara yao ya mechi tatu nchini Marekani.

Partey, 30, ni mmoja wa wachezaji kadhaa wanaowaniwa na Al Ahli kutoka Saudi Pro League.

Baada ya usajili wa pauni milioni 100 wa Declan Rice kutoka West Ham wiki iliyopita, ilionekana kana kwamba Partey angeruhusiwa kuondoka.

Mchezaji huyo amejiunga na Arsenal kutoka West Ham
Mchezaji huyo amejiunga na Arsenal kutoka West Ham © Arsenal

Partey alijiunga na Arsenal akitokea Atletico Madrid mwaka 2020 na ameoneka kuwa mchezaji muhimu sana kwa klabu hiyo japokuwa amekuwa akikabiliwa na changamoto za majeraha.

Alicheza mechi 33 za ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita, akifunga mabao matatu, walipomaliza katika nafasi ya pili mbele ya Manchester City.

Thomas Partey amekuwa akikabiliwa na majeraha japokuwa amekuwa mchezaji muhimu sana kwa Arsenal
Thomas Partey amekuwa akikabiliwa na majeraha japokuwa amekuwa mchezaji muhimu sana kwa Arsenal © AFP - IAN KINGTON

Arsenal wanasema wanaimarisha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa ligi kuu pamoja na mechi za klabu bingwa barani Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.