Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-KASHFA-ZUMA-UCHUNI

Afrika Kusini: Bunge lakataa kung'olewa kwa Rais Jacob Zuma

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameponea kung'olewa Jumanne hii, Aprili 5 kufuatia ombi lililotolewa na upinzani baada ya hukumu ya Mahakama ya Katiba iliomshtumu rais wa nchi hiyo kukiuka katiba.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, aponyoka kura ya kutokua na imani naye.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, aponyoka kura ya kutokua na imani naye. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Chama tawala cha cha ANC, ambacho kinamuunga mkono rasmi Jacob Zuma, kimetumia idadi kubwa ya Wabunge wake kwa kukataa kutimuliwa mamlakani kwa kiongozi huyo.

Kulikua kunahitajika theluthi mbili ya kura ili ombi hilo likubaliwe.

Mahakama ya kikatiba ilibaini kwamba Rais wa Afrika Kusini amevunja Katiba kwa kukataa mpaka sasa kulipa sehemu ya fedha za umma zilizotumiwa kwa kukarabati makazi yake binafsi.

Huu ulikua utaratibu mwengine wa kung'olewa mamlaka uliokua ukimkabili Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Maandamano dhidi yake ya hivi karibuni hayakuwa na nguvu. Tangu Alhamisi, Machi 30, wito wa kujiuzulu umeongezeka ikiwa ni pamoja na katika upande wa chama chake.

Maveterani kadhaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi wametoka katika ukimya ili kumuomba Rais Zuma kujiuzulu kufuatia uamuzi wa Mahakama ya kikatiba ambayo ilitoa uamuzi kuwa hatua ya Rais Zuma ni kinyume na katiba katika kusimamia kashfa ya Nkandla.

Hata hivyo, katika uamuzi wake, Mahakama ya kikatiba pia imewashtumu wabunge kwamba walishindwa kuwajibika katika majukumu yao kwa kutouliza shughuli za rais, hasa ukarabati wa makazi binafsi ya rais Zuma katika kijiji cha Kandla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.