Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Donald Trump na Hillary Clinton washinda kura za mchujo New York

Donald Trump amepata ushindi mkubwa katika kura za mchujo kwa chama cha Republican zilizopigwa Jumanne Aprili 19, katika jimbo la New York. Kwa upande wa chama cha Democratic, Hillary Clinton ameibuka mshindi katika kura hizo zilizotangazwa kama muhimu katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa mgombea urais wa Marekani.

Hillary Clinton baada ya ushindi wake katika kura za mchujo kwa upande wachama cha Democratic katika jimbo la New York, Aprili 19, 2016.
Hillary Clinton baada ya ushindi wake katika kura za mchujo kwa upande wachama cha Democratic katika jimbo la New York, Aprili 19, 2016. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump na Hillary Clinton wamethibitisha nguvu zao na kuonyesha ubabe wao katika jimbo la New York. Jimbo muhimu kwa wagombea kwa sababu baada California, jimbo hili ni muhimu zaidi katika suala la wajumbe. Kura za mchujo za Jumanne hii zinaweza kuwa hatua kubwa katika kambi moja kama katika kambi nyingine.

Upande wa chama cha Republican, Bilionea kutoka jimbo la New York, Donald Trump, ameshinda kwa 59.8% ya kura dhidi ya 25.2% alizopata mkuu wa jimbo la Ohio, John Kasich na 14.9% alizopata Seneta kutoka jimbo la Texas Ted Cruz, kulingana na matokeo ya awali ya zoezi hilo.

Mgombea wa chama cha Republican, hivyo, anaongoza zaidi ya mpinzani wake mkuu, Ted Cruz, baada ya kushindwa katika jimbo la Wisconsin.

Katika kambi ya chama cha Democratic, baada ya mashaka mafupi, hatimaye Hillary Clinton, ambaye alikuwa Seneta kutoka jimbo hilo, ameibuka mshindi, kulingana na matokeo pia ya awali. Amekamilisha 57.3% ya kura, wakati ambapo mpinzani wake, Seneta kutoka jimbo la Vermont Bernie Sanders amepata 42.7% ya kura.

Ushindi ambao unamruhusu Hillary Clinton kushinda mchuano huo katika uteuzi wa kuwania kiti cha urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika Novemba 8, 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.