Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA

Morgan Tsvangirai na Joice Mujuru kuungana kwa kumuangusha Mugabe

Viongozi wawili wa vyama vya upinzani nchini Zimbabwe wamekubaliana kuunda umoja kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao nchini humo, baada ya kuweka kando tofauti zao za muda mrefu.

Wanasiasa wawili wa upinzani, Morgan Tsvangirai (kulia) na  Joice Mujuru ( kushoto) waungana kwa kumuangusha Mugabe.
Wanasiasa wawili wa upinzani, Morgan Tsvangirai (kulia) na Joice Mujuru ( kushoto) waungana kwa kumuangusha Mugabe. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi mkuu wa upinzani wa chama cha Movement for Democratic, Morgan Tsvangirai na aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Joice Mujuru wa chama cha National people's Party walitia saini makubaliano hayo siku ya Jumatano.

Morgan Tsvangirai na Joice Mujuru wameonekana kumaliza baadhi ya tofauti zao.Tsvangirai anasema makubaliano yaliyotiwa saini baina ya vyama viwili ni msingi kuelekea kuunda umoja wa vyama kwa ajili ya kupambana na chama tawala Zanu PF cha Robert Mugabe.

Tayari, vyama vingi vidogo vya upinzani vimemuidhinisha Morgan Tsvangirai kuwa mgombea wao wa urais.

Changamoto iliyopo hivi sasa ni kuamua nani kati ya hao wawili ataongoza muungano huo.

Hata hivyo awali rais Robert Mugabe alitoa maneno ya dhihaka kutokana na mipango ya upinzani aliyodai kuungana kumuondoa madarakani.

“Sina hofu na upinzani, na wala hauninyimi usingizi, ” amesema rais Mugabe.

Itafahamika kwamba Mugabe ni mmoja wa marais wa Afrika ambaye anatawala kwa miaka mingi. Rais huyo amekua akikabiliana na upinzani, hasa maandamano ya hapa na pale wakipinga utawala mbaya na mdororo wa uchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.