Pata taarifa kuu
UINGEREZA-Siasa

Uingereza : William Hague ajiuzulu

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza William Hague ametangaza kujiuzulu jumatatu wiki hii jioni kwenye wadhifa wake na kuondoka kabisa kwenye nafasi yake ya ubunge katika chaguzi za mwaka ujao.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza, William Hague ajiuzulu,
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza, William Hague ajiuzulu, REUTERS/Kerim Okten/Pool
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili limetolewa wakati waziri mkuu David Cameron akianzisha zoezi la kulifanyia mabadiliko baraza la mawaziri, ambalo zoezi hilo linatazamiwa kukamilika jumanne wiki hii.
David Cameron aliahidi tangu kitambo kulifanyia marekebisho baraza la mawaziri kabla ya chaguzi za mwaka 2015. Lakini kujiuzulu kwa mmoja kati ya mawaziri wake ambaye alikua akishikilia wadhifa muhimu umewashitua wengi.

William Hague, waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza.
William Hague, waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza. Reuters / Denis Balibouse

William hague ana uzowefu wa kazi kwa zaidi ya miaka ishirini na amekua akiteuliwa kwenye na fasi muhimu kupitia chama chake. William Hague amejulikana sana kupitia wadhifa huu wa waziri wa mambo ya nje, baada ya kujihusisha na utatuzi wa migogoro katika mataifa mbalimbali duniani: Ukraine, Iraq, Nigeria na hivi karibu baada ya mapigano kati ya Israel na Palestina.

Mpaka sasa mtangulizi wake Philip Hammond, ambaye ni waziri wa ulinzi hajaonekana mtu mahari kwa majukumu aliyotekeleza akiwa waziri wa mambo ya nje kama William Hague.

Waziri mkuu David Cameron, anataka kubadili serikali kwa kuwaondoa mawaziri walio na umri mkubwa na kuwateua vijana na wanawake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.