Pata taarifa kuu
UKRAINE-LUGANSK-WAFUNGWA-USALAMA

Jeshi la Ukraine na waasi wabadilishana wafungwa

Jeshi la Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine, wamebadilishana wafungwa Jumamosi Februari 21, kama yanavyobainisha makubaliano yaliyoafikiwa hivi karibuni katika mji wa Minsk.

Maelfu ya wanajeshi wa Ukraine wamepiga kambi karibu na mji muhimu wa Debaltseve.
Maelfu ya wanajeshi wa Ukraine wamepiga kambi karibu na mji muhimu wa Debaltseve. REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi 139 waliokua mikononi mwa waasi wamekabidhiwa jeshi la Ukraine, huku waasi 52 waliokua wakishikiliwa na jeshi wakikabidhiwa waasi wanaotaka kujitengwa kwa eneo la mashariki.

Zoezi hili limefanyika katika uwanja wa mapigano katika mkoa wa Lougansk, mashariki mwa Ukraine.

Mvutano umeendelea kushuhudiwa mashariki mwa Ukraine kati ya vikosi vya Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Jumatano jioni wiki hii, rais wa Ukraine, Petro Porochenko, aliomba kutumwa kwa ujumbe wa askari polisi wa Umoja wa Ulaya chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa katika eneo la mashariki mwa Ukraine.

Viongozi wa Ulaya wanajaribu kutafuta msimamo wa pamoja ambao wanaweza kupitisha kwa kutafutia suluhu mogogoro kati ya pande hizi mbili.

Licha ya mji wa Debaltseve kuanguka mikononi mwa waasi, hali bado ni tete kwenye uwanja wa mapigano.

Rais wa Ukraine aliomba hivi karibuni Umoja wa Ulaya kutuma kikosi cha askari polisi ambacho kitahudumu chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa, na kitahusika na kufuatilia uheshimishwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa Ukraine. Makubaliano ambayo yalitiliwa saini juma lililopita katika mji wa Minsk. Lakini mpaka sasa ombi lake halijapatiwa jibu.

Zoezi la kuondoa silaha za kivita, moja ya makubaliano yaliyoafikiwa katika mji wa Minsk, haliwezi kufana, wakati ambapo vita vitakua bado havijasitishwa katika maeneo yote yanayokabiliwa na mapigano, ameonya Petro porochenko.

Rais Petro Porochenko alikua akiomba kuachiliwa huru kwa raia wa Ukraine ambao wamefanywa wafungwa na waasi, wakiwemo wale waliokamatwa hivi karibuni katika mji wa Debaltseve.

Mapigano ynaendelea pembezoni mwa mji wa Debaltseve licha ya makubaliaono ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa. Maelfu wa wanajeshi wa Ukraine wamezingirwa katika mji huo wa mashariki mwa Ukraine.
Mapigano ynaendelea pembezoni mwa mji wa Debaltseve licha ya makubaliaono ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa. Maelfu wa wanajeshi wa Ukraine wamezingirwa katika mji huo wa mashariki mwa Ukraine. REUTERS/Gleb Garanich

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.