Pata taarifa kuu
UGIRIKI-UTURUKI-ULAYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji wakabiliwa na ajali mbalimbali kwa kuingia Ulaya

Kama kila siku kwa muda wa wiki kadhaa, mamia ya wahamiaji wamekua wakijaribu kuingia Ugiriki wakitokea Uturuki. Hata hivyo wahamiaji hao wanakabiliwa na ajali mbalimbali wanapoingia Ugiriki au nchi jirani.

Wakimbizi wakijaribu kuingia katika kisiwa cha Kos, nchini Ugiriki wakisafiri katika mazingira magumu.
Wakimbizi wakijaribu kuingia katika kisiwa cha Kos, nchini Ugiriki wakisafiri katika mazingira magumu. REUTERS/Alkis Konstantinidis
Matangazo ya kibiashara

Hatari ni kubwa, lakini wahamiaji wako tayari kukabiliana na matatizo hayo ili wahakikishe wameingia Ulaya. Hali hii imeshuhudiwa katika mji wa Bodrum nchini Uturuki, hatua ya mwanzo ya safari ya wahamiaji wanapoelekea katika kisiwa cha Kos, nchini Ugiriki.

Wahamiaji wamekua wakianza safari yao hiyo katika majira ya usiku, wakati bahari inakua imetulia, na  mbali kidogo na vituo vya polisi. Wahamiaji wengi wanaotokea barani Asia, husasan nchini Syria wamekua wakipiga kambi katika mji wa Bodrum, nchini Uturuki wakisubiri kuanza safari yao wakielekea katika kisiwa cha Kos, nchini Ugiriki kabla ya kuingia Ulaya.

“ Ninatengeneza mfuko ambapo nitahifadhi pesa yangu kutokana na maji, ntafanya hivyo hivyo kwa simu yangu na pasi yangu ya kusafiiria ”, amesema mmoja wa wahamiaji hao.

Kwa kuelekea katika kisiwa cha Kos, wahamiaji hao ambao wengi wao ni wakimbizi, wamekua wakisafiri katika mazingira magumu, huku wakitumia boti au matairi, lakini safari zao zimekua zikikumbwa na matatizo mengi. Wahamiaji wengi wamepoteza maisha katika safari kama hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.