Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Jean-Marie Le Pen afukuzwa katika chama cha FN

Kamati tendaji ya chama cha FN kimetangaza Alhamisi jioni wiki hii kwamba kimemfukuza katika chama hicho Jean-Marie Le Pen. Jean-Marie Le Pen, mwenye umri wa miaka 87, mmoja wa waanzilishi wa chama cha FN, aliongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka 40.

Jean-Marie Le Pen, baada ya kusikilizwa na kamati endaji ya chama cha FN, Agosti 20, 2015.
Jean-Marie Le Pen, baada ya kusikilizwa na kamati endaji ya chama cha FN, Agosti 20, 2015. REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

" Jean-Marie Le Pen alikua anakabiliwa na kesi za kinidhamu baada ya kutoa kauli ziliozua utaua kuhusu Shoah ", limesema tangazo hilo la chama cha FN.

Kabla ya kusikilizwa na kamati tendaji ya chama cha FN, Jean-Marie Le Pen alikuwa alitoa wito kwa chama kuungana. Jambo ambalo halikufanyika. Katika taarifa fupi, chama cha FN kimetangaza Alhamisi jioni kufukuzwa kwa kiongozi wa kihistoria katika chama. " Kufuatia mkutano uliofanyika leo, kamati tendaji ya chama cha FN, iliokutana kwa kujadili suala la nidhamu, imetoa na kuamua katika idadi kubwa inayohitajika, kumfuta katika chama Bw Jean-Marie Le Pen kwenye uanachama wa wa chama cha FN ", limesema tangazo hilo.

Jean-Marie Le Pen aliitishwa kwa mara ya kwanza Alhamisi mchana na kamati tendaji ya chama iliyokutana kwenye makao makuu ya chama katika mji wa Nanterre. Alitazamiwa kujibu zaidi ya maswalikumi natano, ikiwa ni pamoja na kauli ziliozua utata kuhusu vyumba vya gesi viliochapishwa katika gazeti la kila wiki la Rivarol na matusi ya mara kwa mara dhidi ya binti yake akiwa pia rais wa chama cha FN, Marine Le Pen na mshirika wake wa karibu Florian Philippot. Wawili hawa hawakuwepo katika mkutano huo, ili isonekani kuwa wameshinikiza kamati hiyo kuchukua uamzi. Baada ya muda wa saa tatu wakijadili hali hiyo, kamati tendaji ulichukua uamzi wa kumfuta katika chama cha FN kiongozi wa kihistoria wa chama hicho Jean-Marie Le Pen.

Kufukuzwa huko kunakuja baada ya miezi mitano ya malumbano ya ndani kati ya baba na binti yake. Mwishoni mwa mwezi wa Mei, kamati tendaji ya chama cha FN ilimsimamisha na kuitisha mkutano mkuu wa chama kupitia njia ya posta ili kumfuta katika nafasi yake kama rais wa heshima wa chama cha FN. Jean-Marie Le Pen aliwasilisha kesi hiyo mbele ya mahakama ambayo ilichukua uamzi wa kumrejesha katika nafasi yake. Adhabu yake ilifutwa katika masuala ya kiutaratibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.