Pata taarifa kuu
CHINA-MDORORO WA UCHUMI-MASOKO YA HISA

Masoko ya hisa yaendelea kuporomoka Shanghai

Siku moja baada ya "Jumatatu ya giza" kwenye masoko ya hisa ya dunia, mdororo umeendelea kushuhudiwa Jumanne asubuhi katika Soko la Hisa la Shanghai lakini katika maeneo mengine makubwa ya kibiashara barani Asia kama vile Tokyo na Hong Kong, kumekua na nafuu.

Ubao unaoonesha jinsi sarafu ya Japan inavyouzwa kwa siku ya leo Jumanne Agosti 25 mwaka 2015.
Ubao unaoonesha jinsi sarafu ya Japan inavyouzwa kwa siku ya leo Jumanne Agosti 25 mwaka 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Shanghai, ambapo Soko la Hisa limeshuka kwa 8.5% imepelekea Jumatatu wiki hii Masoko ya Hisa duniani kushuhudia mporomoko wa 6.41%, ikiwa ni kiwango cha chini kabisa tangu Desemba mwaka jana. Lakini baada ya zaidi saa moja ya kikao, kwenye saa 09:00 usiku (saa za kimataifa), kiwango cha Soko la Hisa cha Shanghai kilishuka hadi 4% kwa pointi 3079.26.

Katika mji mkuu wa Japan, Tokyo, sarafu ya Nikkei, ambayo imeshuka kwa zaidi ya 3% katika biashara ya kwanza Jumanne wiki hii imefuta hasara zake zote za asubuhi, na baada ya masaa zaidi ya mawili ya biashara, sarafu hiyo imepanda kwa kasi na kupata faida ya zaidi 1.5%. hali kama hiyo imeshuhudiwa katika mji wa Hong Kong, ambapo sarafu ya Hang Seng, ambayo ilishuka kwa 0.6% imerudi kupanda na kufikia kwenye mtari wa kijani kwa kupata 1.96% baada ya zaidi ya saa moja ya biashara.

Soko la Hisa la Taiwan, ambalo lilishuka 4.84% Jumatatu wiki hii, sasa limeongezeka na kiwango kikuu cha Soko la Hisa katika Soko la Hisa la Taipei kmepanda hadi kufikia 2.67% leo Jumanne kwenye majira ya saa 9:00 usiku (saa za kimataifa).

Hata hivyo, kushuka kwa uchumi wa nchi ya pili kwa uchumi duniani, kumesababisha mtikisiko katika masoko yake ya kifedha na kushuka kwa sarafu ya Yuan wiki mbili zilizopita. Hali hii imesababishwa na mdororo wa kifedha duniani, ambao unaendelea kuathiri masoko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.