Pata taarifa kuu
EU-UINGEREZA-USHIRIKIANO

Donald Tusk: “maendeleo yapo lakini kuna mengi ya kufanya”

Baada ya mkutano wa Alhamisi hii uliokumbwa na mvutano, viongozi wa Ulaya wanakutana tena Ijumaa hii katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, ili kukubaliana ahadi kuhusu mageuzi yaliombwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, na kufutilia mbali kujiondoa kwa taifa hili katika Umoja wa Ulaya

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron (kushoto), na Rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker (katikati), Februari 18, 2016, Brussels.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron (kushoto), na Rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker (katikati), Februari 18, 2016, Brussels. JOHN THYS/AFP
Matangazo ya kibiashara

“Wakati huu naweza kusema kwamba tumeweza kupiga hatua lakini bado kuna mengi ya kufanya,” Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk, ameonya katika hotuba fupi kabla ya saa tisa asubuhi saa za Ubelgiji Ijumaa hii

Viongozi wa Umoja wa Ulaya, marais na viongozi wa serikali, wamekua wakiondoka katika mazungumzo ya kwanza kuhusu maombi ya mageuzi ya Bw Cameron, yaliofuatiwa na mazungumzo ya kasi kuhusu mgogoro wa wahamiaji unaoligawa bara la Ulaya

Mbele ya washirika wake 27, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza “mkataba wa kuaminika (...) wenye nguvu ambao utaweza kuwavutia raia wa Uingereza wanaounga mkono Uingera kusalia katika Umoja wa Ulaya”. Hii ni fursa ya kutatua tatizo hili la uhusiano kati ya Uingereza na Ulaya ”kwa kizazi kijacho”, amesema Bw Cameron.

Kiongozi huyo kutka chama cha Consevative, anakabiliwa na wimbi la mgawanyiko katika chama chake, ameahidi kuandaa kura ya maoni ya kukubali au la kubaki kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Kura hiyo inatazamiwa kupigwa mwanzoni mwa mwezi Juni, iwapo David Cameron atapata mkataba huo mwishoni mwa mkutano huu wa kilele, ambao huenda kuaendelea hadi Ijumaa hii jioni.

Hata kama wapiga kura kutoka Uingereza wamegawanyika, uwezekano wa kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya unaufanya Umoja huo kuwa na wasiwasi. Umoja ambao unakabiliwa wakti huu na mgogoro wa wahamiaji tangu mwaka 1945.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.