Pata taarifa kuu
MAREKANI-EU

Obama kuzungumzia migogoro Ulaya wakati wa mkutano mdogo

Barack Obama anatazamiwa kutoa Jumatatu hii kutoa hotuba inayosubiriwa kwa hamu na gamu nchini Ujerumani juu ya mahusiano yanayoitwa TTIP.

Rais wa Marekani Barack Obama katika mji wa Hannover, Ujerumani, Aprili 24, 2016
Rais wa Marekani Barack Obama katika mji wa Hannover, Ujerumani, Aprili 24, 2016 AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Rais Obama atatoa wito kwa viongozi wa Ulaya katika mkutano mdogo, wakati ambapo Washington ina wasiwasi kuhusu kudhoofika kwa Umoja huo kutokana na migogoro mingi.

Rais wa Marekani anahitimisha ziara ya siku mbili katika mji wa Hannover, Kaskazini mwa Ujrumani, hatua ya mwisho ya ziara yake ambayo alianzia nchini Saudi Arabia ili kujaribu kuwahakikishia viongozi wa nchi za Ghuba , waliokuwa na wasiwasi na ongezeko la joto la mahusiano kati ya Marekani na Iran. Pia rais wa Marekani alifanya ziara nchini Uingereza ambako alionya dhidi ya nchi hiyo kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.

kudhoofika kwa Ulaya dhidi ya changamoto nyingi zinazoikabili ni chanzo cha kuongezeka kwa wasiwasi kwa utawala wa Marekani: Na jambo jingine ni uwezekano wa kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa ulaya, mogogoro wa wahamiaji, ambao chanzo chake hasa ni migogoro nchini Syria na Libya. Jambo jingine linalotia wasiwasi utawala wa Marekani ni tishio la kigaidi la wanajihadi wa kundi la Islamic State(IS), hali ambayo bado ni tete nchini Ukraine, au kuendelea kwa mdororo wa kiuchumi ambao umekua sugu barani Ulaya.

Mada hizi zitazungumzia katika hotuba ambayo anatazamiwa kutoa Rais Barack Obama mapema Jumatatu hii asubuhi katika maonyesho ya viwanda mjini Hannover, na katika mkutano utakaofanyika mchana na mwenyeji wake, Kansela Angela Merkel na viongozi wa Serikali za Uingereza na Italia, David Cameron na Matteo Renzi, na Rais wa Ufaransa Francois Hollande.

"Rais Obama atajadili mafanikio yaliyopatikana katika maeneo hayo katika miaka ya hivi karibuni na kuonyesha kazi inayobaki kufanywa katika siku zijazo," mmoja wa wasaidizi wake amesema.

Mkutano wa viongozi wa tano ulianzishwa kwa jutihada za Rais wa Marekani, wasaidizi wake wamebaini.

Syria na TTIP katika ajenda ya mazungumzo

Barack Obama anatazamiwa kutangaza Jumatatu hii katika mji wa Hannover kutuma askari 250 wa nyongeza kutoka Jeshi la Marekani nchini Syria kwa lengo la kutoa mafunzo na kusaidia vikosi vya waasi vyenye msimamo wa wastanii, afisa mwaandamizi wa serikali ya Marekani ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.