Pata taarifa kuu
SUDANI-Siasa

Rais wa Sudan atimiza miaka 25 madarakani

Juma hili rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashiri anatimiza miaka 25 toka aingie madarakani nchini humo kwa mapinduzi ya kijeshi huku utawala wake ukiendelea kukabiliwa na changamoto za kijamii na kiuchumi.

Rais wa Sudani, Omar Hassan Al Bashir.
Rais wa Sudani, Omar Hassan Al Bashir. Reuters/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Miaka 25 bado serikali ya rais Bashir inaendelea kukabiliana na makundi ya waasi kaskazini na kusini mwa nchi hiyo hasa kwenye jimbo la Darfur na Kordofan, miji ambayo waasi hawa wamepiga kambi.

Rais wa Sudani Omar al Bashir atimiza miaka 25.
Rais wa Sudani Omar al Bashir atimiza miaka 25. Reuters/Mohamed Nureldin Abdallah

Mbali na changamoto za kiusalama, Serikali yake bado inakabiliwa na changamoto za kiuchumi na kisiasa wakati huu kukishuhudiwa maandamano ya wananchi kupinga hali mbaya ya maisha huku wanasiasa wakidai uwepo wa demokrasia huru.

Wakili Ojwan'g Agina ni mchambuzi wa masuala ya siasa anazungumza nasi akiwa jijini Nairobi nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.