Ufaransa umeitaka serikali ya Burundi kuadhibu watu wanaonyanyasa wengine
Nchi ya Ufaransa imeomba watu wote wanaonyanyaswa wengine kwa sababu za kisiasa nchini Burundi waadhibiwe bila upendelevu kwa lengo la kujiandalia chaguzi zenye haki mwaka 2015.
Imechapishwa:
Cheza - 02:26
Hayo ni matamshi ya balozi wa Ufaransa nchini Burundi Guérit Van Rossoum alipokuwa akihotubia wageni katika maadhimisho ya nchi ya miaka 225 tangu mapinduzi ya tarehe 14 july 1789.
Hayo yakijiri upinzani nchini Burundi umeilalamikia serikali ya rais Nkurunziza kutaka kuingilia mchakato wa kuchunguza jaribio la kumuuwa kinara wa upinzani Charles Nditije wa chama cha Uprona.
Hivi majuzi, Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuwa huenda suala la jaribio hilo likawa njama ya mpinzani mwenyewe, huku msemaji wa polisi nchini Burundi akisikika akisema kuwa uchunguzi huo unaweza ukawekwa tu kwenye kapu.
Katika mkutano na waandishi wa habari jana, Charles Nditije ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha UPRONA ametoa shutuma hizo na kusema kuwa lengo la kuingilia uchunguzi ni ishara tosha kuwa serikali imeshiriki katika jaribio hilo.