Pata taarifa kuu
CAR-Dtotodia-UN

CAR: Michel Djotodia akabiliwa na vikwazo vya UN

Aliye kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati anakabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Michel Djotodia yuko kwenye orodha ya watu ambao wanaweza kuchukuliwa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juma lijalo.

Michel Djotodia katika mkutano uliofanyika Brazzavile, Congo.
Michel Djotodia katika mkutano uliofanyika Brazzavile, Congo. DR
Matangazo ya kibiashara

Michel Djotodia ni mmoja kati ya watu saba ambao wako kwenye orodha ya timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa ambao wanakabiliwa na vikwazo.

Rais huyo wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amewekwa kwenye orodha ya wafanyabiashara haramu wa maliasili pamoja na makampuni mawili ya dhahabu, Badica inayoendesha shughuli zake nchini jamhuri ya Afrika ya Kati na Kardiam nchini Ubelgiji.

Timu hiyo ya wataalamu inamtuhumu Michel DjotodiaDjotodia kudhoofisha mchakato wa Brazzaville na kuendelea kuwashawishi wafuasi wake dhidi ya serikali ya mpito. Wataalam hao wameliomba Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kumuweka kwenye orodha nyeusi ya Umoja wa Mataifa.

Rais huyo wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati anakabiliwa na vikwazo vya kutosafiri na mali zake kuzuiliwa. Uamuzi huo haujachukuliwa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litaamua kama ni muhimu kumchukulia vikwazo Michel Djotodia, kama François Bozizé aliye mtangulia, au kusubiri hadi katika mkutano utakaofanyika mwezi Januari mjini Bangui ili kumshinikiza ajiunge na mpango wa maridhiano ya kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.