Pata taarifa kuu
CAR-SELEKA-Usalama

CAR: mafisa wa juu wa Seleka waunda vuguvugu la kisiasa na kijeshi

Mafisa wa juu wa kundi la zamani la waasi la Seleka walikutana Jumamosi Oktoba 25 na Jumapili Oktoba 26 katika mji wa Bambari katikati ya nchi.

Wapiganaji wa Seleka katika mji wa Bambari, Mei mwaka 2014.
Wapiganaji wa Seleka katika mji wa Bambari, Mei mwaka 2014. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wa kijeshi wamejitenga na uongozi wa Seleka na badala yake wameunda vuguvugu la kisiasa na kijeshi.

Vuguvugu hilo ambalo linajulikana kama Umoja kwa Amani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati UPC, linaongozwa na Ali Darassa ambaye alikua akiongoza jimbo la Bambari kabla ya Seleka kuweka ngome yao kuu katika jimbo hilo mwezi Mei, pamoja na Mahamat al-Khatim.

“ Wakati wa kudumisha amani umewadia.. Hata hivo tunapinga mgawanyiko na mkataba wa usitishwaji mapigano uliyotiliwa saini katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville, amesema msemaji wa vuguvugu hilo”, Nedjad Ibrahim.

“ Tumeamua kushirikiana na kizazi kipya ambacho hakina uhusiano wowote na kundi la Seleka", ameongeza Nedjad, akibaini kwamba uongozi wa kijeshi wa Seleka umeshindwa kudhibiti wapiganaji wake.

UPC imeunda pia tawi la kisiasa. Kiongozi wa tawi hilo ni Habylah Awal, ambaye alikua hivi karibuni msemaji rasmi wa kundi la waasi wa zamani la Seleka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.