Pata taarifa kuu
CAR-SELEKA-Usalama

CAR: waasi wa zamani wa Seleka wagawanyika katika makundi matatu

Kundi la waasi wa zamani la Seleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limegawanyika katika makundi matatu. Hilo ni moja ya masuala yanayogubika mkutano wa kundi moja la waasi hao linaloongozwa na jenerali Zacharia Damane.  

wapiganaji wa zamani wa Seleka wakiwa katika gari, kaskazini mwa mji wa Bangui, Januari 27 mwaka 2014.
wapiganaji wa zamani wa Seleka wakiwa katika gari, kaskazini mwa mji wa Bangui, Januari 27 mwaka 2014. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo ambao umeanza tangu Alhamisi Novemba 20 unafanyika katika kijiji cha Bria mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kundi hilo ambalo linaundwa na jamii ya Goula linamtafuta kiongozi mpya wa tawi la siasa na mwengine atakayeongoza tawi la kijeshi. Makundi mengine mawili, lile linaloongozwa na Nourredine Adam na lingine linaloongozwa na Ali Darras yaliendesha mikutano yao majuma ya hivi karibuni.

Hali hii ya mgawanyiko katika kundi la waasi wa zamani wa Seleka ilianza kushuhudiwa tangu wakati baadhi ya wafuasi wa kundi hilo walishirikishwa katika serikali ya umoja nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Seleka imeendelea kupoteza muelekeo na imani kwa wafuasi wake baada ya kutokea malumbani ya ndani katika kundi hilo, na kupelekea viongozi wake kugawanyika, huku kila mmoja akitafuta kuanzsha kundi lake ili apate umaarufu zaidi. Seleka kwa sasa imegawanyika katika makundi matatu. Kila kundi lina kiongozi na wafanyakazi tofauti.

Kundi linaloongozwa na Zacharia Damane kutoka UFDR limeanzisha mchakato wa kuwatafuta viongozi wake wapya. Hata hivyo jenerali Zundeko wakati mmoja aliwahi kuwa mkuu wa tawi la kijeshi katika kundi hilo jipya la Seleka, anaweza kuwa kiongozi wa kijeshi.

Makundi hayo ambayo kila kundi lina eneo lake ambamo linaendeshea harakati zake, yamekua yakihasimiana mara kwa mara, na kupelekea raia kuyahama makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.