Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Usalama

CAR : kundi moja la Seleka lapinga makubaliano ya kusitisha vurugu

Kundi moja lenye ushawishi mkubwa ndani ya Uasi wa zamani wa Seleka limekataa kutambua makubaliano ya ukomeshwaji wa uhasama uliosainiwa tarehe 23 mwezi Julai jijini Brazaville baina ya wahusika wakuu wa mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya kati.

Wapiganaji wa zamani Seleka, katika mji wa Bria.
Wapiganaji wa zamani Seleka, katika mji wa Bria. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa juma lililopita, Jenerali Joseph Zoundéko, ambaye ni Kiongozi mkuu wa kijeshi wa Muungano wa Seleka ametupilia mbali makubaliano hayo yaliyofanyika chini ya shinikizo kutoka nchi za ukanda na jumuiya ya Afrika ya kati na Umoja wa Mataifa.

Hayo ya kijiri katika kambi za wakimbizi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wanawake wamekua wakifanyiwa maovu malimbali, hususan ubakaji. Nchini Jamhuri ya Afrika ya Akati, mashuhuda wanawanyooshea kidole cha lawama wanajeshi wa kikosi cha umoja wa Afrika Misca kutowatendea haki raia, hususan wanawake wa kambi moja iliyoko katika mji wa Bambari. Wanajeshi hao wamekua wakihusika na vitendo vya ubakaji, kunyanyasa raia, wakati majukumu yao ni kuwalinda raia.

Ushahidi huo unawanyooshea kidole wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika Misca kwa kuwafanya wasichana wa mji wa Bambari watumwa wa ngono. Wasichana hao wamekua wakipewa mkate au dola 1, baada ya kufanyiwa maovu hayo

Hali hiyo inayojiri katika kambi ya Bambari imewatia hofu waangalizi, wakati ambapo kikosi hicho kitakua chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa ifikapo mwezi Septemba.

Wasichana waliyofaniwa vitendo hivyo wananyooshea pia kidolea cha lawama makundi yaenye silaha hususan wanamgambo wa kikristo wa kundi la Anti- balaka kuhusika na vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake na wasichana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.