Pata taarifa kuu
KENYA-ASASI-UGAIDI-USALAMA

Kenya yafuta asasi 510

Viongozi wa Kenya wamechukua uamzi wa kufuta asasi 510, ambazo zinadaiwa kushirikiana na makundi ya kigaidi na zingine ambazo hazikufahamisha akaunti zao za benki, kama inavyoeleza sheria ya Kenya.

Watu wawili, ambao walinusurika katika mashambulizi ya kundi la Al-Shabab yaliyosababisha vifo vya watu 36 katika eneo la Mandera, Desemba 6 mwaka 2014.
Watu wawili, ambao walinusurika katika mashambulizi ya kundi la Al-Shabab yaliyosababisha vifo vya watu 36 katika eneo la Mandera, Desemba 6 mwaka 2014. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo unakuja, baada ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi katika eneo la Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.

Asasi hizo ziliyofutwa ni pamoja na mashirika ya kihisani ya kigeni ambayo yamekua yakiendesha shughuli zao katika aridhi ya Kenya.

Mkurugenzi wa kamati ya uratibu wa mashirika ya kihisani, Fazul Mohamed, amethibitisha kwamba, asasi kumi na tano miongoni mwa asasi hizo zimejulikana kuwa zimekua zikifadhili makundi ya kigaidi, na zingine hazikufahamisha akaunti zao za benki.

" Wanakuja hapa wakiwa na sura za malaika, wakidai kuwa wanakuja kuwahudumia watoto. Lakini wanapowasili Kenya, badala ya kuwahudumia watoto, wanawaua. Tangu mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Ubalozi wa Marekani mwaka 1998, tulikusanya taarifa juu ya mashirika hayo na tulifuatilia kwa karibu utaratibu unaotumia na mashirika hayo mpaka leo wakati ambapo tumerudi kukabiliwa na shughuli za kigaidi katika pwani na kaskazini mashariki mwa nchi", amesema Fazul Mohamed.

Mkurugenzi huyo amebaini kwamba asasi hizo zilifanyiwa uchunguzi na idara za usalama nchini Kenya na za kimataifa.

Uamzi huo unakuja, wakati ambapo serikali ya Kenya iliahidi kuchukua hatua dhidi ya vitisho vya kigaidi baada ya mashambulizi ya hivi karibuni katika eneo la Mandera

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.