Pata taarifa kuu
URUSI-CRIMEA-Diplomasia

Rais wa Urusi asaini sheria inayoitambua Crimea kama sehemu ya Urusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametia saini sheria inayotambua jimbo la Crimea kuwa taifa huru na sehemu ya Urusi.Rais Putin amesema ametambua matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika jumapili iliyopita baada ya wakaazi wa Crimea asilimia 97 kupiga kura ya kutaka eneo hilo kujiunga na Urusi.

Rais wa Urusi Vladimir Putine ametia saini sheria inayotambua uhuru wa kisiwa cha Crimea na kuwa sehemu ya Urusi.
Rais wa Urusi Vladimir Putine ametia saini sheria inayotambua uhuru wa kisiwa cha Crimea na kuwa sehemu ya Urusi. KEYSTONE/Picha ya zamani
Matangazo ya kibiashara

Rais Putin amefahamisha rasmi bunge na serikali ya Urusi kuhusu ombi la kisiwa cha Crimea la kuwa sehemu ya Urusi, ambayo ni hatua ya kwanza muhimu ya kisheria ili kukubalia kisiwa hicho kuwa sehemu ya muungano wa Urusi, imefahamisha leo ikulu.

Rais Putin amefahamisha bunge na baraza la seneti , pamoja na serikali kulingana na katiba ya Urusi, imeendelea kusema ikulu.

Kwa mujibu wa ikulu, rais Putin anatazamiwa baadae leo kujieleza mbele ya bunge na baraza la seneti, viongozi wa majimbo ya Urusi na wawakilishi wa vyama vya kiraia.

Kutokana na hatua hiyo, Umoja wa Ulaya na Marekani wametangaza vikwazo vya kutosafiri kwa maafisa wa ngazi za juu kutoka nchini Urusi na Ukraine akiwemo aliyekuwa rais wa Ukraine Viktor Yanukoych.

Rais Barrack Obama amesema Marekani itaiwekea vikwazo zaidi Urusi, ikiwa itaendelea kuingilia kati maswala ya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.