Pata taarifa kuu
UGANDA

Bunge la Uganda lapitisha sheria kupinga vitendo vya ushoga nchini humo

Bunge nchini Uganda limepitisha muswada wa sheria tata kuhusu kupinga vitendo vya ushoga nchini humo, sheria ambayo sasa itashuhudia mtu atakayepatikana na hatia akitumikia kifungo cha maisha jela.

Waandamanaji mjini Kampala walipoandamana hivi karibuni kupinga vitendo vya ushoga nchini humo
Waandamanaji mjini Kampala walipoandamana hivi karibuni kupinga vitendo vya ushoga nchini humo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo imepitishwa na wabunge bila kupingwa kufuatia mjadala mrefu uliokuwa bungeni kuhusu kupinga vitendo vya ushoga kufanyika kwenye taifa hilo ikiwemo ndoa za watu wa jinsia moja.

wabunge wengi wameonesha kuunga mkono muswada huo huku wachache wakipinga kwa kile walichodai ni kwenda kinyume na haki za binadamu wakati huu ambapo dunia ni yautandawazi.

David Bahati ni mbunge nchini humo nayeye ndiye aliyewasilisha muswada huo bungeni ili ujadiliwe akitaka kutungwa kwa sheria kali ambazo zitazuia vitendo vya ushoga nchini Uganda.

Sheria hiyo imepitishwa wakati huu ambapo wanaharakati nchini Uganda wamekuwa wakiwatetea watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga, ambapo kupitishwa kwa sheria hii kunakuwa ni pigo kwenye harakati zao.

mbunge Bahati anasema hatimaye nchi ya Uganda imeweka historia kwa kupiga marufuku vitendo vya ushoga ambavyo vimekatazwa na mila za kiafrika pamoja na vitabu ya dini kwa hivyo kuidhinishwa kwa sheria hii kutazuia mmomonyoko wa maadili nchini humo.

Kwa mujibu wa sheria hiyo sasa, mtu atakayepatikana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya ushoga atakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani.

sheria hiyo imepitishwa huku ikiwa imepita siku moja tu toka wabunge hao wapitishe sheria ya kukataza wanawake kuvaa mavazi ambao yanakaribia kuonesha maumbile yao ya siri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.