Pata taarifa kuu
YEMEN - ISLAMIC STATE

Kundi la Islamic State lajigamba kutekeleza shambulio jingine jijini Sanaa

Kundi linalojiita Islamic State limejigamba kutekeleza shambulio la kujitoa muhanga hii leo lililogharimu maisha ya watu 28 akiwemo mwanamke mmoja, shambulio ambalo lilitekelezwa dhidi ya jamii ya madhehibu ya Shia wanaochukuliwa na madhehebu ya Sunni kama makafiri. Huu ukiwa ni muendelezo wa mashambulizi ya kundi hilo dhidi ya waumini wa kishia katika kipindi kifupi

Shambulio la bomu Juni 20 juin 2015 mbele ya Musikiti wa washia, Kobbat al-Mehdi, à Sanaa.
Shambulio la bomu Juni 20 juin 2015 mbele ya Musikiti wa washia, Kobbat al-Mehdi, à Sanaa. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo la kuvizia dhidi ya gari lililenga gamilia ya viongozi wa kundi la waasi wa kishia Faycal na Hamid Jayache, wakati watu walipokuwa wamekusanyika kwenye msiba wa mmoja miongoni mwa familia aliefariki duniani kutokana na maradhi.

Mashahidi wanasema baada ya shambulio hilo waasi wa Huthis walizuia eneo nzima na kuacha pekee magari ya kusafirisha wagonjwa.

Gari lilotekwa bomu ndani yake lilipuka na kugeuka chuma. Magari mengine yaliharibika pamoja na makaazi. Watu 28 waliuawa wakiwemo wanawake 8 na wengine 35 waliojeruhiwa, duru za kitabibu zimethibitisha.

Shambulio hilo linakuja wakati huu Yemen ikikabiliwa na kipindi kigumu cha mapigano yanayo wahusisha waasi wa kundi la Houthis walioyateka maeneo kadhaa ya nchi tangu mwaka 2014.

Muungano wa nchi za kiarabu unaongozwa na Saudia Arabia wanaomuunga mkono rais Abd Rabbo Mansour Hadi,aliekimbilia uhamishoni nchini Saudia Arabia wanaendesha tangu March mashambulizi ya anga dhidi ya waasi kuwazuia kuiteka nchi nzima.

Kundi linalojiita Islmic State lilijigamba kwa mara ya kwanza kutekeleza mashambulizi nchini Yeman mwezi March imekiri kuhusika pia katika shambulio hilo kwenye kitovu cha kundi la Houthis katika mjui mkuu Sanaa unaoshikiliw ana waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.