Pata taarifa kuu
YRIA-MAPIGANO

Syria: Aleppo "kukumbwa na maafa ya kibinadamu"

Nchini Syria, mashambulizi na mapigano vimeendelea Ijumaa hii Aprili 29 ikiwa hasa ni mwisho mwa juma ambapo vifo vingi vimeshuhudiwa. Kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), watu wasiopungua 200 wameuawa katika muda wa siku saba ziliyopita.

Afisa wa kikosi cha ulinzi wa raia akimuokoa mtoto aliyenusurika kutoka chini ya vifusi vya nyumba katika eneo lililokumbwa na mashambulizi ya anga mjini Aleppo, Syria, Aprili 28, 2016.
Afisa wa kikosi cha ulinzi wa raia akimuokoa mtoto aliyenusurika kutoka chini ya vifusi vya nyumba katika eneo lililokumbwa na mashambulizi ya anga mjini Aleppo, Syria, Aprili 28, 2016. REUTERS/Abdalrhman Ismail
Matangazo ya kibiashara

Baada ya muda mfupi wa utulivu, mashambulizi yamerudi kushuhudiwa mapema asubuhi. Mashambulizi makubwa katika mji wa Aleppo pia yameanzishwa.

Mashariki mwa mji ambapo waasi wanadhibiti, kituo cha afya kimeshambuliwa kwa mara nyingine tena, siku mbili tu baada ya shambulio mbaya dhidi ya hospitali ya Al-Quds. Mashambulizi hayo ya anga yaliwajeruhi watu wengin na kuharibu majengo ya hospitali hiyo.

Wakati wa wiki iliyopita, kulishuhudiwa kuuongezeka kwa kasi kwa mapigano. Bila shaka, kitovu kinapatikana katika sehemu ya mashariki ya mji.

Makombora yameanza kurushwa katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali. Makombora hayo yamesababisha vifo vingi katika sehemu ya magharibi ya jimbo la Aleppo, kwa mujibu wa televisheni ya serikali.

Ndani ya siku kadhaa, mji wa pili wa Syria umeshuhudia kiwango cha machafuko ambayo haujawahi kushuhudia kwa wiki kadhaa. Hivyo, mkataba wa usitishwaji mapigano uliotangazwa mwezi Februari sasa unaonekana kama kumbukumbu ya mbali.

Kila upande katika uwanja wa mapigano pia unatarajia kuongezaka kwa mapigano na mashambulizi, kwa mujibu wa gazeti la Syria El Watan, lililo karibu na utawala wa Bashar Assad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.