Pata taarifa kuu
SYRIA-OBAMA-MAPIGANO

Syria: mapigano yanaendelea, Obama atuma askari 250

Nchini Syria, mashambulizi katika maeneo yanayokaliwa na watu wengi katika jimbo la Aleppo, Jumatatu, Aprili 25, yamegharimu maisha ya watu 19 na wengine 120 kujeruhiwa, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu la Syria (OSDH).

Raia wakihamishwa baada ya shambulio la anga katika jimbo la Aleppo, Aprili 23 2016.
Raia wakihamishwa baada ya shambulio la anga katika jimbo la Aleppo, Aprili 23 2016. KARAM AL-MASRI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kusini mwa mji wa Damascus, watu kadhaa waliuawa na arobaini wengine kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lilotegwa ndani ya gari katika kitongoji kinachokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia.

Mkataba wa usitishwaji mapigano kwa sasa umesahaulika nchini Syria. Mapigano yanaendelea kurindima katika maeneo mbalimbali nchini Syria, lakini Jimbo la Aleppo ndio linaathirika zaidi na machafuko hayo. Kwa siku tu ya Jumatatu, karibu watu 140 pekee waliuawa na wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya waasi katika maeneo ya magharibi yanayodhibitiwa na majeshi ya serikali. Zaidi ya watu 80 waliuawa katika kipindi cha siku tatu na mamia zaidi kujeruhiwa katika mji wa Aleppo katika mapigano kati ya jeshi na waasi katika maeneo ya yanayokaliwa na watu wengi.

Mashambulizi katika maeneo ya magharibi yalitokea siku moja baada ya kushindwa katika mashambulizi ya pamoja ya waasi na kundi la Al-Nusra Front, tawi la Al Qaeda nchini Syria, dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na majeshi ya serikali. Waasi walipata hasara kubwa kwa kupoteza idadi kubwa ya wapiganaji katika uwanja wa vita.

Machafuko pia yalitokea Jumatatu, karibu na eneo linalokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia la Sayeda Zeinab, kusini mwa mji wa Damascus.

Pentagon iko tayari kutuma askari zaidi nchini Syria

Barack Obama alitangaza mwishoni mwa wiki iliyopita kutuma askari 250 wa Marekani nchini Syria. Askari ambao wataongezwa kwa askari 50 wa vikosi maalum ambao wako tayari nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.