Pata taarifa kuu
SYRIA-UN-MAPIGANO

Watu 20 wauawa katika mashambulizi ya anga Syria

Watu zaidi ya 20 wamepoteza maisha baada ndege ya kivita ya serikali ya Syria kushambulia hospitali moja mjini Aleppo.

Maandamano dhidi ya serikali ya Syria mjini Aleppo, Syria, Machi 7, 2016.
Maandamano dhidi ya serikali ya Syria mjini Aleppo, Syria, Machi 7, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya shambulizi hili, Umoja wa Mataifa umesema hali hii inahatarisha mafanikio ya mazungumzo ya amani kati ya waasi na serikali ya Rais Bashar Al Assad.

Shambulizi hili limesababisha vifo vya wagonjwa na wafanyikazi wa hospitali akiwemo daktari Wasem Maaz, aliyekuwa anawatibu watoto.

Shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka (MSF) linasema watu 14 waliuawa papo hapo wakiwa hospitalini.

Waokoaji wamekuwa wakiwatafuta watu wengine, ambao wanaaminiwa huenda wamekwama katika vifusi vya hospitali hiyo iliyoporomoka baada ya kushambuliwa.

Kwa muda wa wiki moja, zaidi ya watu 200 wamepoteza maisha mjini Aleppo katika mashambulizi yanayoendelea.

Mashambulizi haya yamemsukuma Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhsuu mzozo huu Stafan de Mistura kuitaka serikali ya Marekani na Urusi kusaidia kusitisha mashambulizi haya na kufanikisha mazungumzo ya amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.