Pata taarifa kuu
ZAMBIA-Sheria

Mwanasiasa wa mpinzani nchini Zambia afunguliwa mashtaka baada ya kumfananisha rais na kiazi

Polisi nchini Zambia, wamemkamata na kumfungulia mashtaka mwanasiasa wa upinzani Frank Bwalya kutokana na kumchafulia jina rais wa Zambia, Michael Satta, baada ya kumfananisha na kiazi. Kiongozi huyo wa chama cha Alliance for a Better Zambia, atapewa kifungo cha miaka mitano jela ikiwa atapatikana na hatia.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Bwalya wakati mmoja alikuwa mfuasi wa rasi Satta.

Frank Bwalya, anakuwa mwanasiasa wa pili kujipata matatani baada ya mwansiasa mwingine wa upinzani , Nevers Sekwila Mumba wa chama cha Movement for Multiparty Democracy kuhojiwa na polisi mwaka uliopita kwa kumwita rais Satta mwongo.

Frank Bwalya anadaiwa kumtaja Rais Michael Sata kama "chumbu mushololwa", akimaanisha kiazi, kupitia kwa Redio siku ya Jumatatu.

Katika lugha ya Bemba, tamko hilo lina maanisha kiazi utamu ambavyo humegeka vinapopindwa , maana ya ndani ikiwa mtu ambaye hasikilizi ushauri wa wengine.
Hata hivyo, Bwalya ni kasisi wa zamani na mfuasi wa zamani wa Rais Sata, ingawa sasa anaongoza chama cha muungano wa vyama vya upinzani (Alliance for a Better Zambia (ABZ).

Naibu waziri wa mambo ya ndani, Stephen Kampyongo alisema kwamba, bwana Bwalya alikamatwa kwa kutoa matamshi ya kumharibia sifa Rais Sata.

Upinzani umetaka  Bwalya aachiliwe ukisema kuwa yeye ni mwanasiasa asiyemuogopa mtu yeyote.

Wanasiasa wa upinzani, wamesema kua  matamshi ya Bwalya,hayakua matusi.

Hali kwa sasa nchini Zambia ni ya mvutano kati ya upinzani na utawala.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.