Pata taarifa kuu
GUINEA

Hofu ya Ebola,yailazimu Senegal kufunga mipaka yake na Guinea

Nchi ya Guinea ikishirikiana na mashirika ya afya ya kimataifa inakabiliana na maradhi ya Ebola ambayo yametokea kuwa janga hivi karibuni kwa kuua watu wengi nchini humo.

Mgonjwa wa Ebola akipatiwa huduma nchini Guinea
Mgonjwa wa Ebola akipatiwa huduma nchini Guinea rfi
Matangazo ya kibiashara

Vifo pia vimeripotiwa nchini Liberia na Sierra Leone jambo ambalo limeifanya nchi jirani ya Senegal kuifunga mipaka yake na Guinea.

Mji mkuu wa Guinea Conakry umekuwa katika tahadhari mwishoni mwa Juma baada ya virusi vya ugonjwa wa Ebola ambao umeua watu kadhaa kusini mwa misitu ya nchi hiyo kuthibitika kuenea katika eneo la mji wa bandari lenye watu milioni mbili.

Wale wote walioambukizwa wamekuwa wakitengwa katika hospitali kubwa ya mji mkuu ili kuepusha virusi hivyo hatari kuambukiza watu wengine.
 

Jumla ya idadi ya taarifa za watu wanaohisiwa kuambukizwa ugonjwa huo tangu mwezi Januari hadi tarehe 28 mwezi Machi imefikia 111 na vifo 70 au kiwango cha vifo cha asilimia 63 imeeleza wizara ya Afya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.