Pata taarifa kuu
UN-BURUNDI

Mvutano kati ya serikali ya Burundi na UN

Umoja wa mataifa UN umeeleza kuguswa na kusikitishwa na hatua ya nchi ya Burundi kuamua kumfukuza nchini mwake, mkuu wa kitengo cha usalama kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi (Bnub), kufuatia ripoti yao inayoituhumu serikali ya Burundi kuwapa silaha vijana wa chama tawala cha Cndd-fdd "Imbonerakure" wakati nchi hio inaelekea uchaguzi mkuu.

Serikali ya Burundi imemfukuza mkuu wa kitengo cha usalama kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi (Bnub).
Serikali ya Burundi imemfukuza mkuu wa kitengo cha usalama kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi (Bnub). AFP / Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Burundi imekuja kufuatia kuvuja kwa taarifa ya siri iliyotolewa kwa Serikali ya Burundi, ikionya utawala wa nchi hiyo dhidi ya kutoa silaha kwa vijana wa chama tawala, hali inayohatarisha kutokea kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, amesema Stephane Dujarric msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Tunasikitika na uamzi wa serikali ya Burundi wa kumfukuza afisa wetu Paul Debbie”, ametangaza msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stéphane Dujarric, huku akibaini kwamba kuna uwezekano Umoja wa Mataifa kutoa malalamiko yake kwa njia ya kidiplomasia.

Dujarric amekumbusha kwamba Umoja wa Mataifa umekua ukijadili kwa mara kadhaa na serikali ya Burundi suala la kuwapa silaha vijana wa chama tawala cha Cndd-fdd “Imbonerakure, hususan wakati mmoja wa wajumbe wa Umoja wa Mataifa alipokua akifanya ziara ya kikazi nchini Burundi.

 “Baada ya kuona uzito wa tuhuma hizo, tulijadili suala hilo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na tukaiomba serikali ya Burundi kuanzisha uchunguzi”, ameendelea kusema Dujrric. “Ni kwa serikali ya Burundi kuanzisha uchunguzi kuhusu habari hio, na tunapendekeza iwe hivo”, amesema akisisitiza msemaji huyo wa Umoja wa Matiafa.

Vyombo vya habari nchini Burundi vimekua vikiongelea tangu aprili 11 barua hii ya siri ya Umoja wa Mataifa, ambayo kwa mujibu wake, serikali ya Burundi imekua ikiwapa silaha vijana wa chama madarakani Cndd-fdd “Imbonerakure”, tuhuma ambazo serikali ya Burundi imesema ni “uzushi usiyo kua na msingi”, na kuomba Umoja wa Mataifa kuitaka radhi.

Wakati huo serikali ya Burundi ilitangaza kwamba itamfukuza alhamisi afisa wa kitengo cha usalama cha ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi (Bnub), Paul Debbie.

Umoja wa Mataifa ulitoa onyo kali juma liliyopita dhidi ya serikali ya Burundi, na kuiomba kuwa makaini na kuchukua hatua zinazohitajika kwa kukomesha uhasama wa kisiasa na kujilinda kuwapa silaha vijana wa chama tawala “Imbonerakure” na kuheshimu haki za binadamu.

Umoja wa Mataifa umewatahadhari kuwachukuliya hatua za kisheria hata kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote watakao washawishi vijana katika machafuko.

Hayo ya kijiri waandishi wa habari watatu wa redio mbili zinazojitegemea wanatafutwa na vyombo vya sheria kutokana na habari inayohusiana na ripoti ya Umoja wa Mataifa inayoituhumu na kuionya serikali ya Burundi kwamba inawapa silaha vijana wa chama tawala cha Cndd-fdd "Imbonerakure". Waandishi hao ni pamoja na Alexis Nibasumba muandisha wa habari wa redio Bonesha fm mkoani Bururi kusini mwa Burundi, Alexis Nkeshimana wa redio Bonesha fm mkoani Bubanza mashariki mwa Burundi pamoja na Eloge Niyonzima, muandishi wa redio Rpa mkoani Bubanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.