Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria: mmoja wa viongozi wa Boko Haram akamatwa

Jeshi nchini Nigeria linadai kuwa linamshikilia mmoja wa viongozi wa kundi la Boko Haram nchini humo, anayedaiwa kuhusika na mtandao wa kiintelijensia wa kundi hilo uliohusika na utekaji nyara wa wasichana 200 mwezi Aprili mwaka huu.

Waandamanaji wakiomba kukombolewa kwa wasichana zaidi ya 200 waliyotekwa nyara na kundi la Boko Haram nchini Nigeria.
Waandamanaji wakiomba kukombolewa kwa wasichana zaidi ya 200 waliyotekwa nyara na kundi la Boko Haram nchini Nigeria. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Jeshi limemtaja mtu huyo kuwa ni, Babuji Ya'ari kiongozi wa kamati ya usalama ya vijana anayedaiwa kutumia wadhifa wake huo kufanya kazi za siri za kundi la Boko Haram katika kutekeleza utekaji huo.

Msemaji wa jeshi la Nigeria, Chris Olukolade.
Msemaji wa jeshi la Nigeria, Chris Olukolade. REUTERS/Afolabi Sotunde

Jeshi linasema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu ni hatua muhimu katika uchunguzi wao utakaowezesha kubaini mahali walipo wasichana hao waliotekwa kwenye jimbo la Borno.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa licha ya kiongozi huyu kukamatwa nchi hiyo bado inakabiliwa na changamoto kubwa hasa katika kukabiliana na wapiganaji hao ambao wanaonekana kuwatumia hata baadhi ya wanasiasa kuchochea mzozo huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.