Pata taarifa kuu
TUNISIA-LIBYA-Mapigano

Tunisia : serikali yatishia kufunga mpaka wake na Libya

Serikali ya Tunisia imetishia kufunga mipaka yake na kutopokea wakimbizi kutoka Libya wanaoyakimbia mapigano, iwapo idadi ya wakimbizi hao itaendeleza kuongezeka.

Serikali ya Tunisia yatishia kufunga mpaka wake na Libya ili kupunguza ongezeko la wakimbizi wanaoingia nchini Tunisia wakitokea Libya.
Serikali ya Tunisia yatishia kufunga mpaka wake na Libya ili kupunguza ongezeko la wakimbizi wanaoingia nchini Tunisia wakitokea Libya. AFP PHOTO/ABDERRAZEK KHLIFI
Matangazo ya kibiashara

“Hali ya uchumi wa nchi yetu si ya kuridhisha, kwa hiyo hatuwezi tukakubali kuendelea kupokea mamia kwa maelfu ya wakimbizi wanaoendelea kuyakimbia mapigano kama ilivyokua mwaka 2011, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe viliyouondoa madarakani utawala wa Moamar Kadhafi”, amesema waziri wa mambo ya nje wa Tunisia, Mongi Hamdi.

“Tutafunga mipaka iwapo itahitajika”, ameendelea kusema Hamdi.

Waziri huyo hakutoa idadi kamili ya raia wa Libya ambao wamvuka mpaka wa Libya na kuingia Tunisia kwa kuhofia maisha yao kutokana na mapigano yanayoendelea, huku akisema kwamba raia walioingia hivi karibuni nchini Tunisia wakitokea Libya ni kati ya 5000 na 6000.

Amebaini kwamba ameomba Umoja wa Mataifa kutuma maafisa wake kwenye mipaka ya Tunisa na Libya ili kushuhudia raia wanaoingia nchini Tunisia wakiyakimbia mapigano nchini Libya.

Kuhusu wafanyakazi kutoka Misri na Jordania wanaokimbia Libya, Hamadi amesema kwamba watu hao wanapitia tunisia ili waweze kujielekeza katika mataifa yao.

“Misri na Jordania zimeomba turuhusu raia wao waingiye nchini Tunisia ili waweze kuendelea na safari hadi katika mataifa yao, Kila mtu kutoka mataifa hayo anapaswa kuwa na nauli au tiketi ya ndege, na anapowasili hapa nchini tunamsafirisha moja kwa moja hadi uwanja wa ndege wa Djerba na Gabès, kusini mwa Tunisia", ameongeza Hamdi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.