Pata taarifa kuu
BURUNDI-RWANDA-Haki za binadamu

Maiti katika ziwa Rweru : Burundi na Rwanda zimeanzisha uchunguzi

Maiti zinaendelea kuokotwa katika ziwa Rweru nchini Burundi. Tayari timu ya mseto inayoundwa na viongozi wa ngazi ya chini na askari polisi kutoka Rwanda na Burundi wamejielekeza jumatatu wiki hii kwenye ziwa Rweru.

Edouard Nduwimana, waziri wa Burundi mwenye dhamana ya mambo ya ndani.
Edouard Nduwimana, waziri wa Burundi mwenye dhamana ya mambo ya ndani. assemblee.bi
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wameshuhudia maiti mbili zikiwa zimefungwa ndani ya magunia zikielea kwenye maji ya ziwa. Hadi sasa ni maiti tano ambazo zimeonekana katika eneo hilo kwa muda wa wiki moja.

Habari hii inaendelea kugonga vichwa vya habari nchini Burundi baada ya wavuvi katika ziwa la Rweru, kubaini kwamba tangu mwezi Julai wamekua wakiona kati ya maiti sita na arobaini zikielea kwenye maji ya ziwa hilo, linalopatikana kaskazini mashariki mwa Burundi. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kibinafsi mjini Bujumbura, ni wiki moja sasa tangu watu wapige kelele kuhusu hali hiyo.

Zaidi ya miili 10 ikiwa ni pamoja na wanaume, wanawake na vijana imeonekana hivi karibuni ikielea kwenye ziwa Rweru tangu jumamosi Agosti 23 mwaka 2014, huku baadhi ya miili hiyo ikifungwa kamba.

Akihojiwa na idhaa ya kifaransa ya RFI, juzi jumapili, mwakilishi wa wavuvi katika wilaya ya Giteranyi iliyokaribu na ziwa Rweru, amethibitisha kwamba alijielekeza pamoja na wanajeshi wa majini karibu na mto Kagera ambao unatiririsha maji kwenye ziwa Rweru, wakakuta maiti mbili, ambayo moja ilikua ilifungwa ndani ya mfuko.

Kiongozi wa ujumbe wa Rwanda amebaini kwamba maiti hizo sio za raia wa Rwanda, wala hazitokeyi nchini Rwanda. Kauli hiyo haitofautiani na kauli ya viongozi wa Burundi. Wazairi wa mambo ya ndani wa Burundi, Edouard Nduwimana, ameelezea wasiwasi wake kuhusu maiti hizo, na kuwatolea wito mataifa hayo mawili kushirikiana kwa kuendesha uchunguzi.

“...Mpaka sasa, na kwa mujibu wa ripoti tulizotumiwa na viongozi tawala kwenye ngazi ya chini, tunaweza kuthibitisha kwamba maiti hizo sio za raia wa Burundi”, amesema Edouard Nduwimana...

Wavuvi wanaoendesha shughuli yao katika ziwa Bweru, wameelezea RFI kwamba maiti hizo zimekua zikitokea katika mto Kagera, ambao unatiririsha maji kwenye ziwa Bweru.Tume ya mseto kati ya mataifa hayo mawili imeundwa ili kuanzisha uchunguzi kuhusu miili hiyo inayoendelea kuonekana katika ziwa Bweru.

Waziri Nduwimana ametolea wito mataifa hayo kushirikiana katika uchunguzi : “ Kilicho muhimu tena chenye busara, ni mataiafa haya mawili yaani Burundi na Rwanda kushirikiana, wala kusiweko na kutupiana lawama kati ya Rwanda na Burundi. Wanyarwanda au Warundi wote ni binadamu, na hiyo ndio inasikitisha", ameongeza waziri Nduwimana.

Tayari uchunguzi umeanzishwa, upande wa Rwanda na upande wa Burundi, na nadhani hivi karibuni tutawafikishia matokeo ya uchunguzi huo”, amesema waziri Nduwimana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.