Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-Ugaidi-Usalama

Somalia harakati za Al Shaba zaendelea

Kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka nchini Somalia, limetekeleza shambulizi la bomu katika katika makao makuu ya usalama wa taifa jijini Mogadiscio na kusabisha vifo vya watu 12.

Mpiganaji wa Al Shaba kutoka Somalia.
Mpiganaji wa Al Shaba kutoka Somalia. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Al Shabab imesema ilitekeleza shambulzi hilo kwa sababu wafuasi wake wanazuliwa katika majengo hayo na kuteswa, na miongoni mwa waliopoteza maisha katika shambulzi hilo ni wanagmabo saba na raia wa kawaida watano.

Shambulizi hilo linakuja siku moja tu baada ya jeshi la Somalia likisaiwdiwa na lile la kulinda amani la Umoja wa Afrika AMISOM, kufanikiwa kuchukua ngome ya Al Shabab mjini Bulomarer, Kilomita 160 kutoka mjini Mogadiscio.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Somalia, Mohamed Yusuf, amewaambia wanahabari mjini Mogadishu kuwa Al Shabab walishindwa kufanikiwa kutekeleza lengo lao na badala yake magaidi hao wakajilipua ndani ya gari lao baada ya kukabiliwa vikali na wanajeshi wa AMISOM.

Al Shabab licha ya kuondolewa mjini Mogadiscio wamekuwa wakipanga kushambulia majengo ya serikali katika siku za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.