Pata taarifa kuu
BURUNDI-DRC-Usalama

Jeshi la Burundi laondoka mashariki mwa DRC

Baada ya RFI kushuhudia uwepo wa wanajeshi wa Burundi katika kijiji cha Kiliba Ondes, mashariki mwa Congo na kuthibitishwa na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Congo Monusco, hatimaye wanajeshi hao wameanza kuondoka kwenye ardhi ya Congo.

Wanajeshi wa Burundi wakipiga doria.
Wanajeshi wa Burundi wakipiga doria. Bobby Model/Getty images
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo la kuwaondoa wanajeshi hao limeanza licha ya kuwa hakuna taarifa rasmi ambazo zimetolewa na serikali ya Burundi au Congo.

Jumanne mchana wiki hii, magari ya jeshi la Burundi yamekua yakibeba vifaa na baadhi ya wanajeshi yakivuka mpaka wa Congo na kuingia Burundi. Lakini tangu jana Jumatatu, jeshi la Congo llikua likijiandaa kuweka kwenye himaya yake eneo hilo la Kiliba Ondes.

Mapema leo jumanne asubuhi, maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Congo wamekutana na wanajeshi katika wilaya ya Uvira na kuwaeleza kwamba watatumwa Kiliba katika maeneo yaliyokuayakishikiliwa na wanajeshi wa Burundi.

Kwa mujibu wa mashahidi, mapema leo Jumanne mchana wanajeshi wengi wa Congo wameonekana wakielekea Kiliba. Baadhi ya wanajeshi hao wamewaeleza wakaazi wa Kiliba kwamba wanachukua nafasi ya wanajeshi wa Burundi kwa kuendelea na ulinzi wa eneo hilo.

Zoezi hilo limeendeshwa na uongozi wa majeshi ya pande hizo mbili.

Serikali za mataifa hayo mawili (Burundi na DRC) zimekua zikikanusha kuwepo kwa wanajeshi wa Burundi katika ardhi ya Congo, hata baada ya tume ya Umoja wa Mataifa kuthibitisha taarifa hiyo juma liliyopita.

Hivi karibuni ujumbe wa jeshi la Congo ukiongozwa na naibu mkuu wa majeshi anaye husika na ujasusi, jenerali Delphin Kahimbi, alijielekeza Bujumbura, nchini Burundi. Ziara yake hiyo ilikua kujadili na viongozi wa Burundi namna ya kuondoa wanajeshi hao wa Burundi katika kijiji cha Kiliba Ondes ili jeshi la Congo liweze kuchukua udhibiti kamili wa eneo hilo. Kwa mujibu wa mashahidi wanajeshi hao wa Burundi wamekua katika ardhi ya Congo kwa kipidi cha miaka mitatu.

Jeshi la Burundi lilidai hivi karibuni kwamba lilijielekeza mashariki mwa Congo ili kukabiliana na kundi linalodaiwa kuwa liliasi baada ya chama cha Fnl kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano na serikali ya Bujumbura. Hata hivo bada ya mwaka mmoja ya wanajeshi wa Burundi kuwa katika ardhi ya Congo, hakuna operesheni hata moja ambayo iliendeshwa na jeshi la Burundi katika ardhi ya Congo ya kuwasaka wapiganaji wa kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.