Pata taarifa kuu
EBOLA-UN-BAN-AFRIKA

Ban ziarani katika mataifa yaliyokumbwa na Ebola

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, yuko ziarani nchini Liberia tangu mapema Ijumaa Desemba 19 asubuhi, hatua ya kwanza katika ziara yake Afrika Magharibi katika nchi ziliyokumbwa na Ugonjwa wa Ebola.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, katika makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa nchini Ethiopia, akiongelea kuhusu mlipuko wa Ebola, Oktoba 28 mwaka 2014.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, katika makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa nchini Ethiopia, akiongelea kuhusu mlipuko wa Ebola, Oktoba 28 mwaka 2014. AFP PHOTO / Zacharias Abubeker
Matangazo ya kibiashara

Alhamisi Desemba 18 jioni, Ban Ki-moon alikutana na timu ya Umoja wa Mataifa

inayokabiliana dhidi ya Ebola UNMEER, inayoendesha shughuli zake katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

Baada ya Liberia, Ban Ki-moon, atakua ziarani leo mchana nchini Sierra Leone na Jumamosi Desemba 20 atakua ziarani Guinea na Mali.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO), Ugonjwa wa Ebola ulisababisha vifo vya watu 6900 kwa jumla ya watu 18,500 waliobainika kuwa na virusi vya Ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Anne-Marie Capomaccio, ambaye anashirikiana katika ziara hiyo na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, ziara hiyo ya Ban Ki-moon ni ishara ya kuunga mkono na kutoa salaamu za rambirambi kwa mataifa yaliyokumbwa na mlipuko huo wa Ebola uliyosababisha maafa makubwa barani Afrika, hususan nchi za Afrika Magharibi.

Katibu mkuu amechukua uamzi wa kujionea mwenyewe kazi kubwa inayofanywa na watu, hususan madaktari, wauguzi na wafanyakazi wengine katika maeneo yaliyoathirika na Ebola. Ban ameanza ziara hiyo ili kuonesha jitihada za Umoja wa Mataifa kwa kuhakikisha kuwa Ugonjwa wa Ebola umetokomezwa katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea na Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.