Pata taarifa kuu
TANZANIA-UTAWALA BORA-RUSHWA-SIASA

Rais Kikwete amfuta kazi Profesa Tibaijuka

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amemfuta kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka baada ya kutuhumiwa kukiuka maadili ya utumishi wa Umma kwa kuingiziwa fedha kiasi cha Shilingi 1.65 bilioni kwenye akaunti yake binafsi.

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete. TZ govt
Matangazo ya kibiashara

Rais Jakaya Kikwete alichukua uamzi huo Jumatatu desemba 22 wakati alipokua akikutana kwa mazungumzo na wazee wa moka wa Dar es Salaam.

Miongoni mwa mapendekezo ya Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Escrow Tegeta yaliyofikishwa kwenye Serikali ni pamoja na kuwajibishwa kwa Bodi ya Shirika la umeme (Tanesco), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

“Tumezungumza na Profesa Tibaijuka na tumemuomba aachiye ngazi ili tumteuwe waziri mwingine kwani kutokana na kutowajibika kwake kwa maslahi ya umma,” amesema Rais Kikwete.

Aidha Rais Kikwete amesema katika suala la Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter  Muhongo analiweka kiporo maana bado hajapata ufafanuzi kuhusu tuhuma zinazomkabili hivyo pindi atakapopata ufafanuzi na kujiridhisha ataujulisha umma.

Kuhusu suala la bodi ya Shirika la Umeme Tanesco, rais Kikwete amesema hana shida nalo kwa sababu tayari bodi hiyo imeshamaliza muda wake hivyo ni kama imekwishajifuta yenyewe, na kuongeza kuwa tayari Ikulu imeshapewa taarifa za kumtaka achague bodi nyingine, hivyo ndani ya siku chache bodi mpya ya Tanesco itatangazwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.