Pata taarifa kuu
DRC-BUNGE-UCHAGUZI-SIASA

Kikao cha bunge chakumbwa na vurugu

Bunge nchini Jamhuri ya kidemokrasia limeidhinisha sheriampya ya uchaguzi, nchini humo licha ya wabunge wa upinzani kuzusha vurugu wakati wa kikao cha Bunge Jumatatu wiki hii mjini Kinshasa.

Idadi kubwa ya askari polisi imetumwa Jumatatu Januari 12 wakati upinzani ulikua unajianda kuandamana dhidi ya sheria ya uchaguzi ambayo ilikua inajadiliwa Bungeni. Watu kadhaa walijeruhiwa Jumatatu Januari 12 mwaka 2015.
Idadi kubwa ya askari polisi imetumwa Jumatatu Januari 12 wakati upinzani ulikua unajianda kuandamana dhidi ya sheria ya uchaguzi ambayo ilikua inajadiliwa Bungeni. Watu kadhaa walijeruhiwa Jumatatu Januari 12 mwaka 2015. AFP/Papy Mulongo
Matangazo ya kibiashara

Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unaona kwamba mageuzi ya sheria hiyo ya uchaguzi yatachelewesha kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa rais utaompa nafasi rais wa sasa wa nchi hiyo Joseph Kabila madarakani tangu mwaka 2001 kuendelea kusalia uongozini baada ya kutamatika kwa muhula wake wa tatu na wa mwisho mwaka 2016.

Wabunge wa Kambi ya Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesusia kikao cha Bunge hilo kilicholenga kupitisha mswada wa sheria ya uchaguzi siku ya Jumatatu mjini Kinshasa, huku jeshi la polisi likikabiliana na waandamanaji ambapo watu kadhaa wamejeruhiwa.

Wabunge hao waliosikika wakipiga filimbi zao Bungeni wanaamini kuwa sheria ya uchaguzi iliopo inatosha badala ya kupendekeza sensa kabla ya uchaguzi wa urais na wabunge katika mwaka 2016, jambo ambalo wamelielezea kuwa njama ya kurefusha muda wa utawala wa rais Kabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.