Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Kiongozi wa Chama cha Upinzani Burundi auawa

Kiongozi wa chama kidogo cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kufyatuliwa risasi siku ya jumamosi wakazi wamesema.

Waandamanaji huko Chebitoke Burundi wakipinga raisi Nkurunziza kuwania awamu ya tatu ya uongozi
Waandamanaji huko Chebitoke Burundi wakipinga raisi Nkurunziza kuwania awamu ya tatu ya uongozi AFP PHOTO/ CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Zedi Feruzi, kiongozi wa chama cha (UPD) alikuwa akielekea nyumbani kwake chini ya ulinzi wa polisi katika wilaya ya Ngagara huko Bujumbura ndipo aliposhambuliwa huku mashuhuda wakieleza kuwa mmoja wa askari waliokuwa wakimlinda pia aliuawa.

Washambuliaji hao walitoroka eneo la tukio bila kutambulika wakitumia gari.

Mauaji hayo yanatokea ikiwa Waandamanaji nchini burundi wanaopinga serikali wakiwa katika siku mbili za usitishwaji wa maandamano baada ya takribani mwezi mzima wa ghasia juu ya kupinga uamuzi wa raisi Nkurunzinza kuwania muhula wa tatu wa uongozi.

Mapema jana Mitaa ya jiji la bujumbura lilikuwa kimya huku maduka yakifunguliwa na baadhi ya askari wakifanya doria katika maeneo kuhakikisha usalama.

Hata hivyo Maandamano ya mwishoni mwa juma yalikuwa makubwa zaidi kuripotiwa  ambapo polisi na wanajeshi walikabiliana vilivyo na waandamanaji ambao walitumia mawe na kuchoma matairi moto kukabiliana na polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.