Pata taarifa kuu
MISRI-SHAMULIO-USALAMA

Misri: askari polisi sita wajeruhiwa katika shambulizi Cairo

Askari polisi 6 wamejeruhiwa katika mji wa Cairo, nchini Misri usiku wa Jumatano kuamkia leo Alhamisi katika mlipuko wa bomu lilokua limetegwa katika gari. 

Askari polisi mbele ya jengo la vikosi vya usalama lililoharibiwa na bomu lililotegwa katika gari katika mji wa Shubra kaskazini mwa Cairo Agosti 20, 2015.
Askari polisi mbele ya jengo la vikosi vya usalama lililoharibiwa na bomu lililotegwa katika gari katika mji wa Shubra kaskazini mwa Cairo Agosti 20, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo limelenga kituo cha polisi, wakati ambapo Misri inakabiliwa na wimbi la mashambulizi ya wanajihadi wa Islamic State (IS).

Shambulizi hili limetokea katika wilaya ya kaskazini mwa mji mkuu dhidi ya kituo cha polisi cha mkoa.

" Mtu asiyejulikana alisimamisha ghafla gari lake mbele ya jengo la polisi, na kutimka papo hapo, kisha gari lililipuka ", imesema Wizara ya mambo ya ndani katika taarifa yake.
"Askari polisi 6 wamejeruhiwa ", wizara hiyo imeeleza.

Ukuta unaozunguka jengo hilo la ghorofa nne umeharibika sehemu kubwa na madirisha ya jengo hilo yamengo'lewa, amearifu mwandishi habari wa shirika la habari la Ufaransa AFP aliejielekeza eneo la tukio.

Hakuna kundi ambalo limedai kutekeleza shambulizi hili, kundi lenye mafungamano na Islamic State katika eneo la Sinai, linaendesha mara kwa mara mashambulizi ya mabomu yakiwalenga askari polisi tangu jeshi lilipomuundoa madarakani na kumkamata rais aliyechaguliwa Mohamed Morsi, Julai 3 mwaka 2013. Baada ya tukio hilo wafuasi wengi wa Morsi walikamatwa na wengine kuuawa.

Mamia ya polisi na askari wameuawa katika kipindi cha miaka miwili, hasa katika eneo la jangwa la Sinai, mashariki mwa Misri, ambapo ni ngome ya kundi la Ansar Beit al-Maqdess ambalo lilikubali kuungana na kundi la Islamic State mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.