Pata taarifa kuu
LIBYA-IS-MAFUTA

Mapigano Libya: ghala kadhaa za mafuta zawaka moto

Ghala zisiopungua nne za mafuta ambayo bado hayajasafishwa, zimewaka moto kaskazini mwa Libya, kutokana na mapigano kati ya walinzi wa mitambo ya mafuta na kundi la Islamic State (IS), Kampuni ya kitaifa ya mafuta (NOC) imesema jumatato hii.

Picha iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii Januari 5, 2016 inaonyesha ghala nne za mafuta zikiwaka moto katika mji wa kituo cha mji wa Al-Sedra nchini Libya.
Picha iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii Januari 5, 2016 inaonyesha ghala nne za mafuta zikiwaka moto katika mji wa kituo cha mji wa Al-Sedra nchini Libya. AFP/HO/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yalitokea Jumatatu na Jumanne wakati ambapo Umoja wa Mataifa unajaribu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika nchi hiyo inayokabiliwa na machafuko ambapo kumeendelea kushuhudiwa serikali mbili hasimu, moja ikipiga kambi Mashariki na inatambuliwa na jumuiya ya kimataifa, nyingine inayopiga kambi katika mji mkuu wa Tripoli, zimeendelea kupigania madaraka.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler, amesisitiza tena umuhimu wa Bunge halali la Libya, lilio mashariki mwa nchi hiyo, kupitisha haraka uundwaji wa serikali hiyo, akionya kwamba kuchelewa kwa uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa kutalinufaisha kundi la IS, ambalo tayari limedhibiti mji wa Sirte (kilomita 450 mashariki mwa mji wa Tripoli).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka NOC ya Jumatano hii, ghala nne za mafuta ziliwaka moto Jumatatu kwa sababu ya kuzuka kwa mapigano karibu na mji wa Al-Sedra, kituo kikubwa cha kuhifadhi mafuta nchini Libya, na kile cha Ras Lanuf, kiliyoko mashariki mwa Sirte.

Afisa wa Usalama wa Kampuni ya kitaifa ya mafuta katika mji wa Sirte amebaini kwa upande wake, akiliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba ghala nne za mafuta zimekua zikiwaka moto Jumatano hii katika mji wa Al-Sedra.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.