Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-CHIBOK

Nigeria: raia wamiminika mitaani Lagos

Ni miaka miwili sasa tangu wasichana wa shule ya Chibo, kaskazini mashariki mwa Nigeria kutekwa nyara na wanamgambo wa kundi la Boko Haram. Zaidi ya wanafunzi 250 wasicahana walitekwa nyara usiku wa tarehe 15 Aprili 2014.

Maandamano katika mji wa Abuja baada ya siku 500 ya wasichana wa shule ya Chibok kutekwa nyara.
Maandamano katika mji wa Abuja baada ya siku 500 ya wasichana wa shule ya Chibok kutekwa nyara. © REUTERS/Akintunde Akinleye
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia tukio hilo maandamano yamefanyika Alhamisi hii Aprili 14 katika mji wa Lagos ili kuhamasisha mamlaka ya Nigeria kuhusu hatima ya wanafunzi hawa wasichana na vikao vya maombi vinafanyika nchini kote.

Kundi la Boko Haram liliwateka nyara mamia ya wasichana wengine, ikiwa ni pamoja na karibu 400 katika miezi mitatu ya mwisho wa mwaka 2014 katika kijiji cha Damasak, kusini mwa mpaka wa Niger.

Kwa sasa vijana wengi hasa wasichana wako mikononi mwa magaidi waliodhoofika kijeshi kwa mwaka mmoja sasa, na wanatumia kama ngao.

Wasichana hawa walizuiliwa wakati fulani katika mji wa Gwoza, mji uliochaguliwa na Boko Haram mwezi Agosti 2014 kama mji mkuu wa mkuu wa kundi hili. Jeshi la Nigeria ililiendesha mashambulizi katika mji huo na kwatimua wanamgambo wa Boko Haram, lakini inaonekana kwamba wapiganaji hawa waliondoka na wasichana hawa katika msafara wao.

Baadhi ya wasichana waliofaulu kutoroka wameelezea masaibu wyalio wakuta. Wanabaini kwamba walifanyiwa mateso mengi.

Ni miaka miwili sasa tangu wasicahana 267 wa shule ya Chibok kutekwa nyara na wanamgambo wa kundi la Boko Haram. Mpaka sasa hakuna taarifa kuhusu waliko wasichana hao.

Wengi wanadhani labda wako Chad ama Cameroon. Lakini wadadisi wanabaini kwamba kuna uwezekano mkubwa wengi wao walilazimishwa kuolewa na wapiganaji. Mpaka sasa wasichana 200 hawajapatikana hadi leo.

Hata hivyo maisha yanaendelea kurejea taratibu katika hali ya kawaida mjini Chibok na usalama umeanza kuimarika.

Watu wamekua wakijiuliza : inawezekanaje katika dunia ya sasa kwamba hakuna msichana hata mmoja alieweza kuokolewa?

Kitendo hiki cha Boko Haram cha kuwateka nyara wasichana hawa kililaaniwa vikali kimataifa na kuchochea kampeni ya mitandao ya kijamii iliyojulikana kama "bringbackourgirls" na kuweka wazi udhalimu unaotekelezwa na makundi ya uasi kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Hata hivyo kundi la Boko Haram limetoa ushahidi kupitia video iliyorushwa kwenye runinga ya CNN kwamba wasichana hao bado hai. Zaidi ya wasichana kumi na tano wameonekana wakivaa hijabu nyeusi.

Vitambaa vyekundu vikifungwa kwenye miti kwa kutowasahau wanafunzi wanawake wa Chibok waliotekwa nyara miaka miwili iliyopita, Abuja Aprili 13 2016.
Vitambaa vyekundu vikifungwa kwenye miti kwa kutowasahau wanafunzi wanawake wa Chibok waliotekwa nyara miaka miwili iliyopita, Abuja Aprili 13 2016. REUTERS/Afolabi Sotunde

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.