Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Askari 24 wa Nigeria wajeruhiwa katika shambulio la Boko Haram

Jeshi la Nigeria linasema wanajeshi wake 24 wamejeruhiwa katika makabiliano na kundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo la Borno.

Katika wiki za hivi karibuni, Jeshi la Nigeria limeimarisha usalama kwenye ngome zake kaskazini mwa nchi, hasa katika jimbo la Maiduguri.
Katika wiki za hivi karibuni, Jeshi la Nigeria limeimarisha usalama kwenye ngome zake kaskazini mwa nchi, hasa katika jimbo la Maiduguri. AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa kwa sasa wanajeshi hao wanatibiwa katika hospitali ya kijeshi mjini Maiduguri.

Wapiganaji wa Boko Haram waliwavizia na kuwavamia wanajeshi hao katika mji wa Kareto na kuzua makabiliano hayo makali.

Serikali ya Nigeria imekuwa ikisema inafanikiwa katika vita dhidi ya kundi hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.