Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-UCHUMI

Zimbabwe: Wakulima wazungu waliofukuzwa na Mugabe kufidiwa

Kuanzia mwezi ujao, serikali ya Zimbabwe itaanza kufidia maelfu ya wakulima wazungu ambao walinyang'anywa mashamba kwa nguvu wakati wa mageuzi ya sera ya umiliki wa mashamba yaliyoanzishwa na Robert Mugabe mwishoni mwa miaka ya 2000.

Chamba ya tumbaku, Zimbabwe.
Chamba ya tumbaku, Zimbabwe. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Robert Mugabe, aliwataka wakulima wazungu waliosalia nchini humo kuondoka na kuwaachia mashamba wazalendo wa nchi hiyo.

"Hatuwataki wakulima wazungu, kumiliki mashamba yetu, lazima waondoke,'' Mugabe aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara.

Mrithi wake Emmerson Mnagagwa ameapa kuinua kilimo ikiwa ni moja ya malengo yake makuu katika mageuzi ya kiuchumi. Pia aliwatolewa wito wawekezaji wa kimataifa kuchangia katika kuendeleza uchumi wa nchi hiyo ambao uko hatarini.

Mageuzi ya sera ya umiliki wa mashamba yaliyozinduliwa na Robert Mugabe katika miaka ya 2000 yalisababisha maafa ya kiuchumi. Kwa kuwanyng'anya wakulima 4,000 mashamba yao, rais Mugabe alitaka kurekebisha haki ya kijamii iliyotokana na ukoloni. Lakini hatua yake kuhusu mageuzi katika sekta hiyo ilizua sintofahamu na kupelekea mdororo wa kiuchumi.

Wakosoaji wa Rais Mugabe, wanasema kuwa sera yake kutaka kumiliki mashamba yote yanayomilikiwa na wazungu, ndio ilisababisha kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 2000-2009.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.