Pata taarifa kuu
Zimbabwe_UHURU-SIASA-USALAMA-UCHUMI

Miaka 40 ya uhuru wa Zimbabwe

Wananchi wa Zimbabwe wanaadhimisha miaka 40 tangu taifa lao lilipojipatia uhuru kutoka kwa wakoloni kutoka Uingereza. Lakini licha ya kuwa huru kwa muda mrefu, Zimbabwe inaendelea kukumbwa na hali ngumu ya kiuchumi.

Robert Mugabe, wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa taifa jipya la Zimbabwe(zamani ikiitwa Rhodesia), akikabidhi medali ya uhuru kwa mwanamfalme Charles, Aprili 1980.
Robert Mugabe, wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa taifa jipya la Zimbabwe(zamani ikiitwa Rhodesia), akikabidhi medali ya uhuru kwa mwanamfalme Charles, Aprili 1980. AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya miaka mingi nchi hiyo kuwa chini ya uongozi wa rais wa zamani Marehemu Robert Mugabe na baadaye serikali mpya kuingia madarakani, wananchi wa taifa hilo wanasema hawana cha kusherehekea hasa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.

Raia wengi wa Zibabwe walimlaumu rais Robert Mugabe, mwasisi wa uhuru, na rais wa kwanza wa taifa hilo, kwa kushindwa kuipatia nchi yake uhuru wa kweli.

Robert Mugabe, aliyekuwa Rais wa Zimbabwe tangu mwaka 1980 hadi 2017, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, tarehe 6 Septemba 2019 akiwa katika Hospitali moja nchini Singapore.

Siku kama ya leo, maelfu wangekusanyika katika uwanja wa taifa jijini Harare na kusikiliza hotuba ya rais lakini kutokana na mamabukizi ya virusi vya Corona, sherehe za mwaka huu zimesitishwa.

Tarehe 18 Aprili mwaka 1980 ilikuwa siku iliyojawa na matumaini kwa watu wa Zimbabwe. "Umeshika lulu mikononi mwako na hivyo itunze." Hayo ndiyo maneno ambayo Samora Machel, aliyekuwa rais wa Msumbiji na Julius Kambarage Nyerere, rais wa kwanza wa Tanzania, walimwambia Robert Mugabe siku ambapo Zimbabwe ilipata uhuru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.