Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Zimbabwe: Vita vya kisheria vyaibuka juu ya mwili wa Robert Mugabe

Rais wa zamani wa Zimbabwe, aliyefariki dunia mnamo mwaka 2019 baada ya miaka 37 mamlakani, alizika katika mji alikozaliwa. Walakini, mwezi Mei, kiongozi wa jadi wa eneo hilo, akiombwa na mmoja wakaazi wa mji huo, aliamuru mwili ufukuliwe uzikwe katika Makaburi ya Mashujaa wa kitaifa huko Harare.

Tangu kifo chake mnamo mwezi Septemba 2019, mazishi ya Robert Mugabe yalizua mvutano mkubwa  kati ya familia yake na serikali.
Tangu kifo chake mnamo mwezi Septemba 2019, mazishi ya Robert Mugabe yalizua mvutano mkubwa kati ya familia yake na serikali. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa jadi anabaini kuwa mahali pa mazishi hapakuwa pa heshima kulingana na mila. Watoto watatu wa Bwana Mugabe wanapinga uamuzi huu.

Ni kwa haki gani kiongozi wa jadi wa eneo hilo anawezaje mwenyewe kutoa uamuzi juu ya jinsi Robert Mugabe alizikwa? Hili ndilo swali lililoulizwa na watoto watatu wa rais wa zamani wa Zimbabwe. Wanawakilishwa na wakili Fungai Chimwamurombe, kutoka chama cha mawakili cha Zenas.

Uamuzi wa chifu wa jadi umekumbwa na kasoro nyingi. Hana mamlaka ya kutoa uamuzi kama huo. Lakini Mahakama inawachukulia watoto wa Mugabe kuwa wageni kwa kesi hii. Kwa hivyo, hawana haki ya kukata rufaa juu ya hukumu hiyo. Tunapinga uamuzi huu na tutakata rufaa kwa Mahakama Kuu ya Zimbabwe.

Kuanzia kifo chake mnamo mwezi Septemba 2019, mazishi ya Robert Mugabe yalizua mvutano mkubwa  kati ya familia yake na serikali. Kambi hizo mbili zilikuwa zikivutana kuhusu mahali pa maziko. Kwa sasa kumeibuka mzozo kuhusu kumbukumbu ya rais huyo wa zamani kulingana na mwanahabari huru Xolisani Ncube.

"Kumbuka, Robert Mugabe alipinduliwa kwa mapinduzi mnamo 2017. Na alipokufa, serikali ilipambana ili kuweza kumzika Robert Mugabe kwenye makaburi ya Mashujaa wa taifa. Na leo, ni kana kwamba serikali inataka kutumia mwili wa Robert Mugabe kupata imani ya wafuasi wake. "

Ili kuepusha mvutano wowote wa kisiasa, familia ya rais wa zamani imejipanga kukabiliana na keshi hiyo mahakamani. Septemba 21, itakuwa zamu ya Grace Mugabe, mjane wa Robert Mugabe kutetea kaburi la mumewe mahakamani. Anaomba marekebisho ya hukumu ya kiongozi wa jadi wa eneo alikozikwa Robert Mugabe ambaye anaamuru mwili wa kiongozi huyo ufukuliwe na kuzikwa kwenye makaburi ya Mashujaa wa taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.