Pata taarifa kuu

Mali: Denmark yadai kwamba wanajeshi wake "wamealikwa" Bamako

Mzozo kati ya Bamako na Copenhagen juu ya uwepo wa wanajeshi wa Denmark nchini Mali. Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, serikali ya mpito ya Mali iliomba kuondoka kwa wanajeshi wa Denmark kutoka kikosi cha kupambana na ugaidi cha Takouba.

Kikosi cha kijeshi cha "Takouba" kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa jeshi la Mali katika mapambano dhidi ya wanajihadi kimesimamishwa hadi itakapotangazwa tena.
Kikosi cha kijeshi cha "Takouba" kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa jeshi la Mali katika mapambano dhidi ya wanajihadi kimesimamishwa hadi itakapotangazwa tena. © AFP - DAPHNE BENOIT
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha Takuoba kinaundwa na wanajeshi kutoka nchi za Ulaya chini ya uangalizi wa jeshi la Ufaransa Barkhane. Bamako inaishutumu Denmark kwa kutuma wanajeshi wake "bila idhni yake". Kile ambacho Denmark inakanusha.

Denmark inadai kupokea "mwaliko wa wazi" kwa vikosi vyake maalum. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark inaeleza kwamba "mchango wa Denmark ulikubaliwa na serikali iliyopita ya Mali na, mara kadhaa, na serikali ya sasa ya mpito". Copenhagen inaeleza utaratibu mzima wa utawala uliofuatwa.

Hasa juu ya hadhi ya kikosi hiki kilichowekwa chini ya usimamizi wa jeshi la Ufaransa Barkhane na kutia saini kwenye mkataba wa Sofa - "Makubaliano kuhusu sheria ya vikosi vya majeshi", - uliyowekwa na Ufaransa, kama ilivyo kwa makumi ya nchi zingine za Ulaya ambazo zilikubali kutuma vikosi maalum nchini Mali ili kuchangia katika mapambano dhidi ya makundi ya kijihadi.

Copenhagen inataja mikutano kadha kati ya ubalozi wake na Waziri wa Ulinzi wa Mali, Kanali Sadio Camara, mwezi wa Aprili uliyopita, au hata mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark na mwenzake wa Mali Abdoulaye Diop, miezi minne iliyopita, ambapo mawaziri wa Mali walielezea kwa uwazi kuridhika kwao na kutoa shukrani zao kwa kujitolea kwa Denmark ndani ya kikosi cha Takouba. Denmark inasema kushangazwa na ombi la Mali kutaka kupata makubaliano ya nchi mbili ambayo inachukuliwa kuwa rasmi na kwa upande wake inaomba ufafanuzi.

Jumanne jioni, kwenye kituo kimoja cha habari na kwa lugha ya Kibambara, Waziri Mkuu Choguel Maïga alikumbusha kwamba Denmark, kama mtu yeyote anayetaka kuja nchini, lazima wawe na makubaliano Na Mali.

Kikosi cha Denmark, ambacho kiliwasili hivi karibuni, kinaundwa na watu 90. Jumatano hii, walikuwa bado wakisubiri huko Menaka, kaskazini mwa Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.